MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE TANZANIA
HomeJamii

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nane wa Majaji Wanawake uli...






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nane wa Majaji Wanawake ulioandaliwa na Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) unaofanyika kila baada ya miaka miwili na mkutano wa mwaka huu ulikuwa na kauli mbiu isemayo Kuongoza njia kufikia hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati.


Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akihutubia wakati wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa PSPF Golden Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mhe. Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar,Mhe. Othman Makungu,akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).
 
 


Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania Jaji Imani Aboud akitoa Salaam za ufunguzi wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)
 


Sehemu ya waliohudhuria wakiwa makini katika kuchukua yale yaliosemwa na Mhe. Makamu wa Rais wakati wa uzinduzi wa mkutano wa nane wa Chama Cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza Majaji na Mahakimu wanawake kote nchini kupambana ipasavyo katika kukabiliana vitendo vya rushwa,unyanyasaji kijinsia na rushwa ya ngono ili kusaidia wanawake kupata haki zao za msingi bila kubaguliwa katika jamii. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati anafungua Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA).

Makamu wa Rais pia ameonya kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono inayofanywa na baadhi ya watendaji wenye madaraka na kusema tabia hiyo  ni mbaya na lazima ikomeshwa mara moja katika jamii.

Amesema kuwa vitendo hivyo vya rushwa ya ngono huzuia na kukwamisha juhudi za wanawake kufikia huduma za kijamii na za kiserikali ipasavyo ikiwemo elimu, ajira na haki kwa ajili ya ustawi wa wanawake.

Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekishukuru Chama cha Dunia cha Majaji Wanawake (IAWJ) kwa mchango na msaada wake kwa TAWJA katika programu ya miaka mitatu ya kupambana na matumizi mabaya ya madaraka na rushwa ya ngono.

Makamu wa Rais pia ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria, Shirika la UN Women na wadau wengine wa TAWJA kwa kuunga mkono mapambano ya aina zote za ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini. 

Amesema elimu ya haki za Binadamu iliyotolewa na Chama hicho imeleta badiliko kwa wengi kwa njia ya mafunzo na machapisho na jitihada hivyo lazima ziongezwe ili huduma hiyo iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi kote nchini.

Amesisitiza wanachama wa Chama cha TAWJA waendelee kutoa msaada katika kuwasaidia wanawake na watoto ambao wanakandamizwa kwa kunyimwa haki zao katika jamii ili waweze kupata haki zao nchini.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Chande Othman amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa mkakati wa uimarishaji wa shughuli za mahakama nchini unaendelea vyema lengo likiwa ni kutenda haki kwa wananchi kote nchini bila ubaguzi.Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TAWJA) “Kuongoza njia kufikia hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati”.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE TANZANIA
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE TANZANIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimsA8E8OpGFBoSzMepSve5jfoXV7tRmXAZV9282fH5NUSjwSma9rh0IU_kFZhOmQxkMc8l8ZdM_wtUiZbZmcWjlBgp5k8zAx9ZD02_eH7cw4txB4p_SbwmYqNEGIjGXIuYI8M-xp4WzRg/s640/11.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimsA8E8OpGFBoSzMepSve5jfoXV7tRmXAZV9282fH5NUSjwSma9rh0IU_kFZhOmQxkMc8l8ZdM_wtUiZbZmcWjlBgp5k8zAx9ZD02_eH7cw4txB4p_SbwmYqNEGIjGXIuYI8M-xp4WzRg/s72-c/11.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa-nane.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa-nane.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy