Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Kilombero Ujenzi Wa Daraja la mto kilombero ni moja ya vitu vinavyotajwa na vilivyopo katika vinywa ...
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Kilombero
Ujenzi Wa Daraja la mto kilombero ni moja ya vitu vinavyotajwa na vilivyopo katika vinywa Vya wakazi wa eneo hili kukuza uchumi wa Wilaya ya Malinyi na Ulanga.
Ujenzi Wa daraja hilo ambao umekamilika kwa asilimia 80 unatarajiwa kuongeza matumaini makubwa kwa wakazi wa Wilaya hizi mbili, ambazo kwa kiasi kikubwa hutegemea biashara ya mchele Kama ndio uti wa mgongo wa mapato.
Kwa upande wake Mkurugenzi Chalinze wa Malinyi, Marcelin Ndimbwa amesema daraja hilo litafungua Biashara upya kwa kasi kutokana maeneo hayo kufikiwa na vyombo vya usafiri kwa saa 24 .
Amesema Wilaya hizi mbili zilikuwa zinadumaa kutokana na kutofikika kwa urahisi ,lakini kwa muonekano huo kila mmoja ana matumaini na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mmoja wa wakazi wa Ifakara Said Lumisha amesema kila mfanyabiashara ana imani na serikali ya awamu ya tano, kwani kila mmoja anahitaji kusafirisha Mchele mwingi, ila wanashindwa kutokana na tatizo la miundo mbinu ikiwemo kivuko.
Ametaja kuwa mzigo wa kupakiwa kwenye Lori,unapakiwa nusunusu kutokana na kivuko kutokuwa na uwezo mkubwa, lakini siku chache maroli makubwa yataweza kufika mpaka Ulanga na Malinyi kwa urahisi na zaidi.
Ametaja uwepo Wa daraja hilo kuwa utafungua njia ya basi kwenda Songea kupitia Malinyi kwani njia ni fupi kuliko kuzunguka Iringa,Anataja kuwa watu Wa mikoa ya kusini wakihitaji kwenda Dodoma hawatakuwa na haja ya kupitia Dar es salaam kwani daraja hili likikamilika mambo mengi ya kimaendeleo yatafunguka,
Muonekano wa daraja la Kilombero kwa mbali ambalo inaelezwa kwa asilimia 80 limekwishakamilika
Sehemu ya ujenzi wa daraja hilo muhimu ukiendelea
COMMENTS