Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiwa wanaelekea katika kituo cha wazee na wasiojiweza cha Sarame Magugu, Wilaya...
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiwa wanaelekea katika kituo cha wazee na wasiojiweza cha Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, kutoa msaada wa shuka na vyandarua na vyakula mbalimbali , dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni yaliyotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation.
Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akimkabidhi, mmoja kati ya wazee wa kituo cha wazee na wasiojiweza Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, Aaron Owiso, ambapo waliwakabidhi wazee hao mashuka, vyandarua, vyakula, dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.
Mzee Maalim Masaja (kushoto)anayelelewa katika kituo cha wazee wasiojiweza cha Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, akipokea mfuko wenye mchele kwa niaba ya wenzake toka kwa Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, ambapo msaada huo ulitolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa wazeeikiwa ni pamoja na mashuka, vyandarua, vyakula, dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.
COMMENTS