RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA
HomeJamii

RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la ...

ELIMU YA KODI NI MUHIMU KWA KILA MMOJA WETU - MHE. SAMIA SULUHU HASSAN
WANAWAKE KANISA LA PENTEKOSTE WAOMBA AMANI ILIYOPO NCHINI IDUMISHWE
VIJANA DAR ES SALAAM WAANZISHA KLABU ZA MABADILIKO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI








Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili kuagwa Mhandisi Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani Katavi, kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida)
 
 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
 

Askari polisi Mkoani Singida wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
 
 

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. 
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016).  
 
 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi. 
 
 
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake.
 

Wananchi waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba.
  
Na Mathias Canal

Mwili wa Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe.

Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
 
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa  Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
 
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi, Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA
RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2nLEFhX_shyphenhyphenF_17Y-5wzuH2mmTlvLgiYanx1RadQ08XOLQ_7JHiGG5XnsGUP4PglLdQE3SWzDvAU_XbnvJ3cfdFtHQChDDkBhlhhLOhh1yIJVnDcVMfiwlJ_clq_FPj9Fb4iK3fIj28U/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2nLEFhX_shyphenhyphenF_17Y-5wzuH2mmTlvLgiYanx1RadQ08XOLQ_7JHiGG5XnsGUP4PglLdQE3SWzDvAU_XbnvJ3cfdFtHQChDDkBhlhhLOhh1yIJVnDcVMfiwlJ_clq_FPj9Fb4iK3fIj28U/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/rc-mtigumwe-aongoza-waombolezaji-kuaga.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/rc-mtigumwe-aongoza-waombolezaji-kuaga.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy