Na Ismail Ngayonga MAELEZO Dar es Salaam 4.12.2016 MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amewata Viongozi wa Dini na Watan...
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dar es Salaam
4.12.2016
MKUU
wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amewata Viongozi wa Dini na Watanzania
kuendelea kumuombea Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kurejesha
misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma iliyoachwa
na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Anasema
katika kipindi cha mwaka mmoja wa Utawala wa Rais John Pombe Magufuli, Serikali
ya Awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo katika kupiga vita rushwa, ufisadi
na kusimamia nidhamu na miiko ya Uongozi katika utumishi wa Umma.
Hayo
yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka
wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi kuelekea katika
maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara.
“Ndani
ya Rais Magufuli anaonekana, Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mstari wa mbele
katika kukemea hadharani vitendo vya uvunjifu wa maadili ya mtumishi wa umma
ikiwemo rushwa na ufisadi” anasema Mtaka.
Kwa
mujibu wa Mtaka anasema hatua zinazoendelea kuchuliwa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma ikiwemo mapambano
dhidi ya rushwa na ufisadi ni jambo la kupongezwa, kwa kuwa limelenga katika
kuwakumbusha watendaji kuwa Uongozi ni dhamana.
Alisema
kuwa hatua zinazochuliwa na Rais John Pombe Magufuli, zinaendelea kuongeza
heshima ya Viongozi wa Tanzania katika medani ya kimataifa ya kusimamia
nidhamu, maadili na miiko ya Uongozi ambayo imetekelezwa katika kipindi chote
cha miaka 55 ya uhuru.
Anaongeza
kuwa, hatua hizo zilizofikiwa na Viongozi hao ni changamoto kwa Viongozi Vijana
waliopo nchini kuendelea kuheshimu misingi iliyoachwa na waasisi wa taifa, na
hivyo kuiwezesha Tanzania kuendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo katika siku
za usoni.
Mtaka
alisema Kiongozi wa Umma ni kioo na kiunganishi katika jamii anayoiongoza,
hivyo ni wajibu wa kila kiongozi wa umma kujenga taswira chanya ya kiutawala
katika kuwahudumia wananchi kwa kutambua kuwa dhamana ya kiongozi ndio tumaini
la watawaliwa.
“Katika
siku za hivi karibuni tumeshudia sekta binafsi zikichukua watumishi waaandamizi
kutoka Serikalini, hiki ni kiashiria kuwa nidhamu na maadili ya kazi
yameimarika kwa kiasi kikubwa sana Serikalini” alisema Mtaka.
Akifafanua
zaidi Mtaka alisema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya
Awamu ya tano pamekuwepo na mageuzi makubwa katika utendaji na uwazi wa
shughuli mbalimbali za Serikali, hatua iliyosaidia kuokoa kiasi kikubwa cha
fedha kilichokuwa kikipotea katika miaka ya nyuma.
COMMENTS