NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, NGERENGERE WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya...
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, NGERENGERE
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu wa Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, wamepongeza uamuzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF
na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wa kuunganisha nguvu na kuwekeza kwenye
mradi wa kiwanda cha sukari, Mkoani Morogoro.
Pongezi hizo walizitoa kwa nyakati tofauti wakati wa mikutano ya
hadhara na wananchi wa kijiji cha Kidunda, Kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro
mwishoni mwa wiki.
Mawaziri hao ambao walikuwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya
mradi huo utakaosimamiwa na kampuni ya Mkulazi Holding, iliyobuniwa na Mifuko
hiyo kutekeleza mradi.
“Ninawapongeza, Mfuko wa PPF na NSSF kwa kuitikia mwito wa
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli, kwa uamuzi wenu
wa kuunga mkono mipango ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa
viwanda, kwa kuunganisha nguvu na kuwekeza kwenye mradi huu.” Alisema Dkt.
Mpango.
Waziri huyo alihimiza taasisi hizo kufanya haraka kukamilisha
upembuzi yakinifu, ili utekelezaji kamili wa mradi ufanyike.
Dkt Mpango aliwataka wahandisi kuhakikisha wanatoka maofisini ili
kukagua ujenzi wa miundombinu inayoambatana na mradi huo ikiwemo barabara
inayojengwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT kuelekea eneo la mradi “Ile barabara ndio itatumika kusafirisha
bidhaa mbalimbali kutoka na kuelekea kiwandani ni vyema kusimamia
kikamilifu” alisema Dkt Mpango huku akikisisitiza Kampuni ya SUMA JKT
kutekeleza mradi huo kwa kiwango cha ubora ili kulinda imani ya Serikali kwa
makampuni ya umma katika utekelezaji wa miradi yake mbalimbali.
Waziri Dkt. Mpango pia aliwapongeza wanakijiji kwa kuupokea mradi
kwa ari ya hali ya juu, na kwamba serikali itahakikisha suala la fidia
linakamilika kwa haraka ili kuepusha mivutano wakati tayari mradi
umekwishakamilika.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, naye
aliipongeza Mifuko ya NSSF na PPF kwa uamuzi wake wa kuwekeza kwenye kiwanda
hicho ambacho. “Kwa kweli nia ya serikali ni kutengeneza ajira kwa wananchi
wetu, naomba watekelezaji wa mradi huu kuanza kuainisha mapema aina ya
rasilimali watu watakaohitajika kwenye mradi huu ili serikali ianze kuwaanda
vijana wa kitanzania kukamata ajira kwenye kiwanda hiki kikubwa.
Awali Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe,
akizungumza wakati wa mkutano huo aliwashukuru NSSF na PPF kwa kuleta mradi huo
katika mkoa wa Morogoro ambapo mradi huo utaenda sambamba na ujenzi wa huduma za
kijamii ambapo Dkt Kebwe aliwataka vijana wa eneo hilo kufanya kazi na
kuchangamkia mradi unaokuja badala ya kuwategemea wanawake na wazee katika
shughuli za uzajishaji.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, akihutubia wanakijiji wa kijiji cha Kidunda, Kata ya Mkulazi, Tarafa ya Ngerengere mkoani Morogoro wakati wa ziara yake na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama.(wakwanza kulia). Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mkulazi Holding, Bw. Ca
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akihutubia
wanakijiji wa kijiji cha Kidunda
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Bi. Jenista Mhagama (watatu
kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kulia), Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara,
(wane kulia), na Mshauri wa Mradi wa Mkulazi, Bw.Suleiman Talqwa,wakiangalia
ramani ya mradi huo.
Baadhi ya wanakijiji waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya wanakijiji waliohudhuria mkutano huo.
Mawaziri hao na ujumbe wao wakikagua
ujenzi wa miundombinu ya barabara itokayo Ngerengere kwenda eneo la
mradi, unaotekelezwa na kampuni ya SUMA JKT
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe, akihutubia
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akisalimiana na
wanakijiji.
Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Mh. Omary Mgumba akizungumza jambo na mawaziri hao kwenye eneo la mradi.
COMMENTS