Disemba 24, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa Bwana Godfrey Sinyangwe (kushoto) pamoja na Bi.Esther Kiluma (kulia), baada ya ...
Disemba 24, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa Bwana Godfrey Sinyangwe
(kushoto) pamoja na Bi.Esther Kiluma (kulia), baada ya kufunga ndoa
takatifu katika Kanisa la Saint Nicholas Jimbo Kuu la Mwanza chini ya
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Lazaro Manjelenga aliyesaidiana na
Mchungaji Joseph Samwel.
Zifuatazo
ni baadhi ya picha zikionesha matukio katika hafla ya ndoa hiyo
iliyofanyika usiku wa kuamkia leo, ukumbi uliopo Bugando Jijini Mwanza.
#BMG
Maharusi wakikata keki
Maharusi wakilishana keki, kwa upendo kabisa
Best man wa bwana harusi, Kabuji Noah (kushoto) pamoja na Best lady wa bi.harusi, Huruma Ntangu (kulia) wakilishana keki
Mshereheshaji, MC Lama, akifungua shampaini kwa ustadi wa hali ya juu.
Ndugu, jamaa, marafiki na wageni waalikwa wakiwapongeza maharusi.
Wazazi wa pande zote mbili wakiwa neno la wosia kwa maharusi.
Ndugu, jamaa, marafiki na wageni waalikwa wakitoa zawadi kwa maharusi.
Kapu la bibi kama kawaida.
Msosi ulipikwa kwa ustadi mkubwa.
Maharusi wakilishana chakula.
Wazazi wakipata chakula.
Ni wasaa wa kufungua mziki.
Burudani ikiendelea.
Hafla
hii imefana sana, shukrani kwa wote waliofanikisha akiwemo Mwenyekiti
wa sherehe, Erica Elias. BMG inawatakiwa kila la kheri kwenye ndoa
yenu, Godfrey Sinyangwe pamoja na Esther Kiluma.
Tazama picha za ndoa HAPA
COMMENTS