AGGREY&CLIFFORD YASAIDIA WATOTO WENYE MAZINGIRA MAGUMU
HomeJamii

AGGREY&CLIFFORD YASAIDIA WATOTO WENYE MAZINGIRA MAGUMU

Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakiwasili katika kituo cha Sadeline. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya Aggrey&Clif...







Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakiwasili katika kituo cha Sadeline.


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Cobus van Zly (kulia) na Mkurugenzi wa huduma za Matangazo,Oliver Mutere (katikati) wakikabidhi baadhi ya zawadi kwa watoto wenye mazingira magumu kwenye kituo cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni kwa Msimamizi wa kituo hicho,Sarah Kitainda wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi na kucheza na watoto hao mwishoni mwa wiki.


Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni,Benedicto Mutayoba akipokea zawadi kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Martin Kirangu wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi kwa watoto na kucheza nao mwishoni mwa wiki,aliyembeba ni mama wa mtoto huyo,Grace Thomas.

Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni,Maulid Rajab akipokea zawadi kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Ndeshi Rajab
Mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Nia van Aswegen (kulia) akiwapatia zawadi watoto Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline
Mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey& Clifford, John Alexander akimkabidhi msaada wa mfuko wa vyakula mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Sadeline.

Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakiwa wamewabeba baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Sadeline
Mfanyakazi wa Aggrey&Clifford,Nadah Dhiyebi akicheza na watoto wa kituo cha Sadeline
Aggrey&Clifford yasaidia watoto wenye mazingira magumu
---
Kampuni ya matangazo na ukuzaji wa masoko ya Aggrey&Clifford mwishoni mwa wiki imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mazingira magumu kituo cha Sadeline kata ya Mbezi Juu ambapo pia baadhi ya wafanyakazi wake walishiriki kucheza na watoto hao kwa ajili ya kuwapatia faraja katika msimu huu wa sikukuu.

Akiongea wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Matangazo ya Biashara wa Aggrey&Clifford,Oliver Mutere, alisema kuwa msaada huo wa nguo na chakula na vifaa vya kusomea ni kwa ajili ya kuwapatia faraja watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu.

“Moja ya sera ya kampuni yetu ni kusaidia shughuli za kijamii ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii ndio maana katika kipindi hiki tumeonelea kuna umuhimu wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata hii ya Mbezi Juu”.Alisema.

Mutere alisema mbali na kutoa msaada wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wamekuwa na utaratibu wa kujitoa na kutoa muda wao kwa ajili ya kusaidia kazi za kijamii “Kutokana na sera hii baadhi ya zawadi hizi zilizotolewa zimetokana na michango ya wafanyakazi”.

Mratibu wa kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Sadeline ,Sarah Kitainda,alishukuru kwa msaada huo ambao alidai kuwa umeleta faraja kwa watoto hao hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya.

“Kwa niaba ya kituo hiki natoa shukrani kwa kampuni ya Aggrey&Clifford kwa kuwakumbuka watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa kata hii ya Mbezi na ni matumaini yangu kuwa mtazidi kushirikiana nasi kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotukabili kuwalea watoto hawa katika siku za usoni.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AGGREY&CLIFFORD YASAIDIA WATOTO WENYE MAZINGIRA MAGUMU
AGGREY&CLIFFORD YASAIDIA WATOTO WENYE MAZINGIRA MAGUMU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCN3_wHPg74xYsUcq-wV6F8vKWYN2HHtRoeIQdBlO4zhamr5J7yqfNQgsqI5HUzAn-7fsqBYXRd8Sd-fnYZWk0PIF0s2Oc6JJjMft_sewLMuUZ8pbiaPeOCg5PTYdwVQEFEFR_bi48SHI/s640/AGGREY+MSAADA+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCN3_wHPg74xYsUcq-wV6F8vKWYN2HHtRoeIQdBlO4zhamr5J7yqfNQgsqI5HUzAn-7fsqBYXRd8Sd-fnYZWk0PIF0s2Oc6JJjMft_sewLMuUZ8pbiaPeOCg5PTYdwVQEFEFR_bi48SHI/s72-c/AGGREY+MSAADA+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/aggrey-yasaidia-watoto-wenye-mazingira.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/aggrey-yasaidia-watoto-wenye-mazingira.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy