Rais wa IRMCT, Bw. Theodor Meron akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, hapo siku ya Jumatano, Ripoti ya ...
Rais
wa IRMCT, Bw. Theodor Meron akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, hapo siku ya Jumatano, Ripoti ya utendaji kazi wa Matawi ya
Mahakama za Kimataifa za Kesi za Masalia zinachokua nafasi ya iliyokuwa
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) na Mauaji
ya halaiki yaliyotokea katika iliyokuwa Yugoslavia ya zamani ( ICTY. Bw.
Meron alitumia pia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano wa hali na mali katika ujenzi wa majengo yanayochokua nafasi
ya ICTR majengo hayo yamejengwa katika eneo la Lakilaki Mkoani Arusha.
.Mwakilishi
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akizungumza
wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti ya utendaji kazi wa IRMCT ambapo
alimshukuru kwa namna ya pekee Msajili wa IRMCT Bw. John Hopkins kwa
uongozi wake na ushirikiano ambao ameonyesha katika ujenzi wa majengo
mapya huko Lakilaki lakini pia katika kusimamia kipindi cha mpito na
makabidhiano kutoka ICTR kwenda IRMCT.
Na Mwandishi Maalum, New York
Umoja
wa Mataifa kwa mara nyingine tena, umeishukuru Serikali ya Tanzania kwa
kusaidia kwa hali na mali ujenzi na hatimaye kuelekea ukamilishwaji wa
Majengo mapya ambayo yatatumika kwa shughuli za iliyokuwa Mahakama ya
Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) ambayo ilihitimisha
majukumu yake mwaka jana.
Shukrani
hizo zimetolewa siku ya jumatano na Bw.Theodor Meron, ambaye ni Rais wa
Mahakama za Kimataifa za Kesi za Masalia na Utunzaji wa kumbukumbu na
nyaraka zote muhimu za zilizokuwa Mahakama za Kimataifa
zilizoshughulikia mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda na Yugoslavia ya
zamani ( IRMCT).
Bw.
Theodor Meron alikuwa akiwasilisha Ripoti yake ya Nne kuhusu IRMCT mbele
ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa . Ripoti ambayo imeanisha maendeleo
ya kipindi cha mpito kutoka ICTR na ICTY kwenda IRMCT kazi ambayo
amesema inakwenda vizuri ingawa kumekuwapo na changamoto kadhaa.
“Wakati
ninapowasilisha ripoti hii, nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za
dhati kabisa kwa mchango mkubwa na ushirikiano ambao tumeupata kutoka
serikali ya Tanzania, takribani wiki tatu zijazo majengo hayo
yatazinduliwa rasmi baada ya kuwa yamekamilika”. Akasema Bw. Meroe
Baadhi
ya changamoto hizo kwa upande wa iliyokuwa ICTR ni pamoja na
kutokamatwa hadi sasa kwa watuhumiwa watatu ambao inaelezwa wapo
mafichoni. Ni
pili ni mahali pa kuwapeleka watu ambao ama wamekwisha maliza kutumikia
vifungo vyao na kuachiwa huru. Watu hao wamekosa nchi ya kuwapokea na
hadi sasa bado wanaendelea kuishi nchini Tanzania.
Na kwa
sababu hiyo, Rais wa IRMCT ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kutoa
ushirikiano wa kuwachukua watu hao ambao hawana mahali pa kwenda na kwa
wale walioko mafichoni nchi ambazo wamejificha watoe ushirikiano kwa
kuwafichua na kuwakamata ili hatimaye sheria iweze kuchukua mkondo wake
Kwa
upande wake, Tanzania kupitia Mwakilishi wake katika Umoja wa Mataifa,
Balozi Tuvako Manongi, amesema Tanzania inakaribisha kuhitimishwa kwa
ujenzi kwa ujenzi wa makazo mapya ya iliyokuwa ICTR katika eneo la
Lakilaki ndani ya wakati na kwa bajeti iliyopangwa.
“Kwa
namna ya pekee tunampongeza Msajili wa Mahakama, Bw. John Hopkins kwa
uongozi wake na ushirikiano wake ambao umewezesha kukamilisha hatua hii
muhimu sana”. Akasisiza Balozi.
Aidha
kukamilika kwa majengo hayo na ambayo yapo katika ardhi ya Tanzania ni
heshima na fahari kubwa na ya kipekee kwa Tanzania na wananchi wake
kutokana na jukumu kubwa iliyobeba ya kuwa mwenyeji wa Mahakama ya
Kimataifa ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda kwa niaba ya Jumuiya ya
Kimataifa.
Balozi
Manongi pia amepongeza uratibu uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa kupitia
Ofisi ya Mshauri wa Sheria, Ofisi ya Msajili na the Hegue ya
kuhakikisha kwamba, pamekuwapo na utaratibu mzuri wa kurithishana kutoka
ICTR kwenda IRMCT. Na kwamba kazi hiyo haikuwa nyepesi.
Akizungumzia
kuhusu kazi za IRMCT, Balozi amesema, Tanzania ingependa kuona Taasisi
za Kitaifa zinawezeshwa ili ziweze kushughulikia kwa ukamilifu, haki na
usawa na kwa kuzingatia sheria za kimataifa kesi zinazopelekwa kwenye
Taasisi hizo za kitaifa.Aidha
akasema uzoefu ambao umepatikana kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na
ICTR pamoja na ile ya ICTY ni vema ukatumika kama mfano katika Mahakama
nyingine za Kimataifa.
Kwa
upande wa mashahidi, Tanzania imesisita umuhimu wa mashahidi kulindwa na
kuhakikishiwa usalama wao dhidi ya vitisho mara baada ya kutoa
ushahidi.Kuhusu
watu walioachiwa huru baada ya kukamilisha vifungo vyao na bado wapo
nchini Tanzania. Tanzania imeungana na wazungumzaji wengine katika
mkutano huo wa kutaka pawepo na majadiliano ya kina ya kuangalia namna
gani ya kuwasaidia watu hao.
Vile
Tanzania imetoa wito kwa nchi zile ambazo zinahisiwa kwamba
zinawahifadhi watuhumiwa watatu ambao wapo mafichoni na wanatakiwa
kufikishwa katika vyombo vya sheria kutoa ushirikiano ili hatimaye haki
itendeke.Watuhumiwa
ambao wametajwa kuwa walihusika kwa namna moja ama nyingine katika
mauaji ya Kimbari nchini Rwanda na wapo mafichoni hadi sasa ni Augustin
Bizimana, Felicien Kabuga na Proitas Mpiranya.
Kwa
mujibu wa Ripoti iliyowasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, watuhumiwa hao watakapopatikana kesi zao zitafanyika katika
Mahakama hiyo mpya nchini Tanzania.Uamuzi
kwa kuwa na matawi ya IRMCT huko Arusha na the Hague, Uholanzi
unatokana na maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia
azimio nambari 1966 la mwaka 2010.
Kupitia
Azimio hilo Baraza la Usalama liliamua kwamba, baada ya kumalizika
rasmi kwa ICTR ( 2015) na ICTY ( 2017) Tanzania ambayo ndiyo ilikuwa
mwenyeji wa ICTR itapewa jukumuu la kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka zote
muhimu za iliyokuwa ICTR ikiwa ni pamoja na kumalizia kesi zitakazokuwa
zimebaki. Huku the Hague ikiwa na dhamana hiyo hiyo kwa kazi zilizokuwa
za iliyokuwa ICTY.
Mahakama
za Kimataifa za Rwanda na Yugoslavia ambazo zimefanya kazi kubwa ya
kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa karibu wote waliohusika na
matukio ya kutisha ya ukiukwaji wa haki za binadamu ziliazishwa mwaka
1990 na Umoja wa Mataifa.
COMMENTS