SBL YAMZAWADIA MTEJA WA BIA YA PILSNER PIKIPIKI MPYA
HomeBiashara

SBL YAMZAWADIA MTEJA WA BIA YA PILSNER PIKIPIKI MPYA

Meneja Chapa wa Bia ya Pilsner, Isamba Kasaka  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa kukabidhi zawadi...

STANBIC BANK YAJA NA AKAUNTI YA HATUA
TIGO YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA TUMIA TIGO PESA NA USHINDE
HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE MAAFURU NYUMBA YA TEMBO YAZIDI KUVUTIA WATALII













Meneja Chapa wa Bia ya Pilsner, Isamba Kasaka  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa kukabidhi zawadi kwa  mshindi wa pikipiki mpya iliyotolewa kwa  Shindano la kunywa bia ya Pilsner  lililofanyika jijini Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki  linalojulikana kama “Pilsner Lager Nguruma Party.”  Pembeni yake ni Meneja Biashara  Mipango na matukio Pwani na Dar es salaam Lulu Mduma katika hafla iliyofanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

Mshindi wa shindano la “Pilsner Lager Nguruma Party. Simon Jonasi aliyejishindia zawadi ya pikipiki akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuonesha furaha yake  mara baada ya kutangazwa mshindi ,Kulia kwake ni Meneja Chapa wa Meneja Chapa wa Bia ya Pilsner, Isamba Kasaka akimsikiliza kwa makini ,Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

Meneja Chapa wa Bia ya Pilsner, Isamba Kasaka akimkabidhi funguo ya pikipiki mshindi wa shindano  la “Pilsner Lager Nguruma Party. Simon Jonas (mwishoni kushoto) na katikati ni Meneja Biashara  Mipango na matukio Pwani na Dar es salaam Lulu Mduma katika hafla  iliyofanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es Salaam.


Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.




Mshindi wa shindano la “Pilsner Lager Nguruma Party. Simon Jonasi aliyejishindia zawadi ya pikipiki akiwa amepozi juu ya pikipiki yake mara baada ya makabidhiano katika hafla iliiyofanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.



Dar es Salaam, Novemba 21, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetoa zawadi ya pikipiki mpya  yenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa mkazi wa jijini Dar es Salaam aliyeibuka kuwa mshindi wa shindano la kunywa bia ya Pilsner  lililofanyika jijini Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki  linalojulikana kama “Pilsner Lager Nguruma Party.”
Akizungumza katika mkutano wa waanndishi wa habari alipokabidhi zawadi hiyo Meneja Chapa wa Bia ya Pilsner, Isamba Kasaka  aliielezea pikipiki hiyo kama zawadi kubwa kufuatia kuwepo kwa matukio mfululizo ya promosheni yanayofanywa na kampuni hiyo katika maeneo tofauti yanayotumika kwa vileo jijini.
 “SBL  imekuwa ikiendesha maonesho ya burudani ya bia ya Pilsner Lager katika mabaa yaliyoteuliwa ndani ya jiji  ikiwa na lengo la  kuwashukuru na kuwazawadia wateja wake wa bia hii. Katika mashindano, tumekuwa  tunawauliza  kuigiza mngurumo wa Simba  na hatimaye mshindi anachanguliwa na wateja wenyewe,” alisema Kasaka.
Meneja wa bia hiyo  alibainisha kuwa  zawadi nyingine kadhaa  zinatolewa  wakati wa matukio  hayo miongoni mwake zikiwa  ni pamoja na  fulana za Pilsner (T-shirts), bia za Pilsner za bure, Skafu za Pilsner (bandanas). Alisema kuwa  tukio hilo limekuwa  linahusisha maonesho mubashara (live) kutoka kwa wasanii wa ndani  na kuongeza, “yote hayo ni katika kuwaongezea hamasa wateja wetu ili kufurahi na kuburudika.”
Naye mshindi huyo, Simon Jonas aliishukuru SBL kwa zawadi hiyo  na kutoa wito kwa wanywaji wa  bia  waendelee kuifurahia Pilsner  ili waweze kupata nafasi ya kutimiza ndoto yao ya  kuendesha pikipiki kupitia promosheni.
 Pilsner ni moja ya bia maarufu nchini na kote Afrika Mashariki. Bia hiyo  ilizalishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1842 mjini Pilsen Jamhuri  ambako ilipata jina lake  ikiwa na kilevi cha asilimia tano.  Bia hiyo kwa bei ya rejareja ni shilingi 1,600 kwa chupa ya mililita 500 na hivyo kuifanya wateja wengi  kumudu kuinunua.


Mwisho
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SBL YAMZAWADIA MTEJA WA BIA YA PILSNER PIKIPIKI MPYA
SBL YAMZAWADIA MTEJA WA BIA YA PILSNER PIKIPIKI MPYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbMjsX5x5c_CvC_3c8-6mGf7ZfC-yicYpk3JLFPeY35Uq46WkvvLnNjXPXeOvlOSBCAw6_a-rIU7vtOGV__OHvaHF42C5GQFP0ttKtKKyPEac6IxjbR5-c7rea5_P3UNBncQ3kqpwFBVA/s640/IMG_0394.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbMjsX5x5c_CvC_3c8-6mGf7ZfC-yicYpk3JLFPeY35Uq46WkvvLnNjXPXeOvlOSBCAw6_a-rIU7vtOGV__OHvaHF42C5GQFP0ttKtKKyPEac6IxjbR5-c7rea5_P3UNBncQ3kqpwFBVA/s72-c/IMG_0394.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/sbl-yamzawadia-mteja-wa-bia-ya-pilsner.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/sbl-yamzawadia-mteja-wa-bia-ya-pilsner.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy