Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wakazi wa Mbagala katika ziara yake ya siku kumi ndani ya jiji la...
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wakazi wa Mbagala
katika ziara yake ya siku kumi ndani ya jiji la Dar Es Salaam,katika
kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Katika
ziara hiyo RC Paul Makonda amewataka wazazi kuchunguza muenendo wa tabia
za watoto wao ili wasije wakajihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo
kujiunga na vikundi vya uhalifu maarufu kama Panya Road, vinginevyo
wazazi hao watachuliwa hatua za kisheria kwa uzembe wa kutokulea watoto
wao katika maadili mema.
Sehemu ya
umati wa Wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa Paul Makonda,alipofika kuzungumza nao na kusikiliza kero zao na
hatimae kuzitafutia ufumbuzi,ambapo wakazi hao pia walipata wasaa wa
kuuliza maswali ya masuala mbalimbali yanayowahusu na kuzieleza kero
walizonazo katika maisha yao ya kila siku.
RC
Makonda akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Msingi
Mbande,jijini Dar ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake katika
wilaya ya Temeke,ambapo Paul Makonda amewataka wazazi kuwa na wajibu wa
kuwasimamia na kuwachunguza watoto wao katika suala zima la kujijenga
kimaadili na kuondokana ama kuepula kufanya mambo yaliyo kinyume na
maadili,vinginevyo serikali itawachukulia hatua wazazi hao.
Akifafanua
zaidi RC Makonda ameeleza kuwa kwa watoto wote waliochini ya umri wa
miaka 18 wote kwa pamoja na wazazi wao watawajibishwa kwa mujibu wa
sheria na kusisitiza kuwa anahitaji kuiona DAR MPYA ambayo kila
mtanzania atakuwa na uhuru wa kufanya mambo yake bila kubughuziwa na mtu
yeyote au kuhofia vitendo vya uhalifu.
Pia
amewataka wanafunzi wa shule hiyo kuwa wasikivu kwa wazazi wao, walimu,
viongozi wa dini na watu wote ili waweze kutimiza malengo na wajitahidi
kusoma kwa bidii kwani kufanya hivyo ni kumuunga mkono Rais John Pombe
Magufuli katika adhima yake ya kuboresha elimu, katika hatua nyingine RC
Makonda amezindua madarasa matatu katika shule hiyo, yaliyojengwa kwa
ufadhili wa Rais Magufuli.
RC
Makonda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vyumba vya madarasa
yaliyojengwa kwa fedha za Rais Dkt John Magufuli,ndani ya Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke,leo jijini Dar.
COMMENTS