PUMA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA DUNIANI KWA KUTUMIA NDEGE 22 ZA ZAMANI

 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, moja y...









 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, moja ya picha ya ndege  22 za zamani zitakazotua nchini Novemba 28, mwaka huu, kwa mashindano ya 'Vintage Air Rally' yenye lengo la kutangaza utalii. Ndege hizo zilitengenezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.Kushoto ni  Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari  (hawapo pichani) Dar es Salaam, Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambamo Mashindano ya Ndege 22 za zamani  'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitatua na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii.  Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange.

 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (katikati) akizungumza katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, kuhusu  maandalizi wa mashindano ya Ndege 22 za zamani  'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitakazotua nchini Novemba 28 na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii.  Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange na Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.

 Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.akijibu maswali ya wanahabari

 Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mafuta ya Ndege ya kampuni hiyo, Andrew Lauwo (kulia)  akifafanua jambo katika mkutano huo

Mkutano ulivyokuwa

Puma Energy
Tanzania Ltd



Taarifa Kwa umma
Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambayo ni sehemu ya Puma Group, Kampuni ya kimataifa inayojishughulisha usafishaji mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta yaliyosafishwa tayari kwa matumizi, inayofuraha kujulisha umma kuwa itakua mfadhili mahsusi  katika  mashindano ya anga yanayohusisha ndege za zamani kwa mwaka 2016.
Vintage Air Rally inahusiaha ndege za zamani za miaka ya 1920 na 1930 ambazo zinarushwa na marubani wenye
uzoefu mkubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiruka kukatisha Afrika kuanzia kisiwa cha Crete Ugiriki hadi Cape town Afrika ya Kusini. Shindano hili lilianza tarehe
12/11/2016 kule Crete, Ugiriki na safari yote itachukua siku 35
  katika jumla ya nchi 10 ambazo ni Ugiriki,
Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya, Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika ya Kusini.
Shindano hili linalengo la kutahini ujuzi wa marubani husika,  na wakati huohuo kuchangisha fedha kwa ajili ya mashirika ya Kimataifa ya hiari UNICEF, Bird life International and Seed Bombing. Sisi kama Puma tunasikia fahari sana kuwa sehemu ya uvumbuzi huu wa ajabu. 
 Kampuni ya Puma Energy inayofuraha kuwa mwenyeji wa mashindano haya.   Ndege zinazotumika katika aina hii ya
mashindano huwa zinahitaji aina maalumu ya matengenezo kwa kuzingatia umri wake pamoja na teknolojia iliyotumika. Tumejikita katika kuendela kufanya vyema na pia kuwa na uhakika wa uapatikanaji wa bidhaa ya mafuta na tunafuraha kutoa mchango wetu katika kuhakikisha kwamba mashindano yanayafanyika vyema. Jukumu
letu katika kusaidia
kuendeleza utalii ndani ya
nchi yetu linabaki kuwa sehemu muhimu sana katika masula yetu ya kijamii kama
kampuni katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku
, Alisema Philippe Corsaletti, Meneja Mkuu wa Puma Enery Tanzania.
Vintage Air Rally watatua Tanzania (KIA) tarehe
28/11/2016 wakitokea uwanja wa ndege wa Wilson Nairobi. Marubani watakua na muda mzuri wa kutembelea mbuga zetu za wanyama kama sehemu ya safari yao. Hili
pekee pia litasaidia katika kuweka utalii wa nchi yetu katika mtizamo wa kimataifa Zaidi kwani shindano hili linafuatiliwa na maelfu ya watu katika maeneo mbalimbali duniani.
 Kampuni ya Puma Energy Tanzania imejiandaa kabisa
kupokea ugeni huu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma zote za kujaza mafuta ili kuhakikisha urukaji ulio salama. Ndege hizi zinatumia mafuta aina ya Avgas ambayo kwa sasa ni kampuni ya Puma pekee inayotunza hapa nchini. Timu ya watu wetu imejiandaa kupokea na kuhudumia msafara mzima katika kiwanga cha juu cha ubora na ufanisi. Uwepo wa bohari zetu za mafuta ya ndege katika maeneo mbalimbali nchini unafanya iwe rahisi kuhudumia ndege hizo ambao msafara huu
utapita.
Kwa hapa Tanzania, Vintage Air Rally Aircrafts zitajaza
mafuta Kilimanjaro, Arusha, Dar es salaam, Zanzibar, Dodoma, and Songwe kabla ya kuelekea Zambia ambapo watapokelewa na kuhudumiwa na wenzetu wa Puma Zambia.Tanzania itaweka historia kwa kuwa moja ya nchi chache duniani ambapo mashindano haya yatapita.
“Tunawakaribisha wananchi wote katika tukio hili la kihistoria wakati ndege za Vintage zitakapokua zikipita maeneo yenu na kutumia fursa hii kuendeleza utalii”, Alisema Ndugu Philippe.

Kuhusu njia itakayotumika:
Njia
inayotumika ni sawa kabisa na ufuatishaji wa safari ya shirika la ndge la Imperial ya mwaka 1931 “safari ya Afrika” ambapo ndege itakua ikiruka chini kupitia Nile kutokea kongo hadi Khartoum, kupitia nyanda za juu za Ethiopia, uwanda wa chini wa Kenya,  na hatimaye sehemu yenye changamko sana ya Afrika Mashariki.  Baada ya hapo itaondoka tena kupitia Kilimanjaro hadi Serengeti, na hatimaye hadi kwenye visiwa vya marashi ya Zanzibar na hadi chini Zaidi, kupitia Zambia, juu ya maporomoko ya Victoria, hadi Bulawayo Zimbabwe. Siku za mwisho za safari hii ndefu inayohitaji pumzi nyingi itawafikisha Botswana na Afrika ya Kusini - Capetown ambapo utakua mwisho wa safari Kampuni ya Puma Energy ni kampuni ya kimataifa ya viwango vya kati ambayo imejikita katika kusafisha
mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta masafi kwa watumiaji katika zaidi ya nchi 45 duniani. Puma Energy iliingia Tanzania mwaka 2012 na hadi sasa inaongoza katika  soko na pia kampuni pekee yenye uwepo katika viwanja vinane hapa Tanzania  ambavyo ni Kilimanjaro, Zanzibar, Songwe, Mwanza, Tabora, Dodoma, Arusha, na Julius Nyerere.

Philippe Corsaletti
Meneja Mkuu.



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PUMA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA DUNIANI KWA KUTUMIA NDEGE 22 ZA ZAMANI
PUMA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA DUNIANI KWA KUTUMIA NDEGE 22 ZA ZAMANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjoQo0M_0rfAMHL5GdV0A0QTz4n3e8n3ZzKtd1ZBPPc1jLQAmtkyc8MVSb4EaS1FPHX4D-G76oaA6lUXDeze3mjc_Tja6pTipbF7sMPF8PFftSW6Mbq1aYjRaSqxq0C5wSDk14SfTvHRgw/s640/01.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjoQo0M_0rfAMHL5GdV0A0QTz4n3e8n3ZzKtd1ZBPPc1jLQAmtkyc8MVSb4EaS1FPHX4D-G76oaA6lUXDeze3mjc_Tja6pTipbF7sMPF8PFftSW6Mbq1aYjRaSqxq0C5wSDk14SfTvHRgw/s72-c/01.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/puma-kutangaza-utalii-wa-tanzania.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/puma-kutangaza-utalii-wa-tanzania.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy