PRECISION AIR YAANZA SAFARI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.
HomeBiashara

PRECISION AIR YAANZA SAFARI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.

Ndege aina ya ATR namba 5H-PWE mali ya Shirika la ndege la Precision Air ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege ulio...









Ndege aina ya ATR namba 5H-PWE mali ya Shirika la ndege la Precision Air ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege uliopo ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti ikiwa na wageni 45 kutoka nchini Afrika Kusini waliofika nchini kwa ajili ya shughul za utalii.
Baadhi ya Wageni wakishuka kutoka katika ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika uwanja huo wa ndege katika Hifadhi ya Serengeti.
Gari la kikosi cha zima moto likiwa kando ya uwanja huo .
Wageni waliowasili katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti wakiwa katika picha ya pamoja. 
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza jambo na Rubani wa ndege Benjamini Malui mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (mwenye kofia) akiwa na Crew ya Ndege ya Precision Air mara baada ya kutua katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
Magari ya kubeba watalii yakiwa yameegeshwa kando ya uwanja wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Tafa ya Serengeti yakiongojea kubeba watalii walioshuka kwenye ndege ya Precision Air.
Madereva wa magari hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Muonekano wa kundi la Nyumbu na wanyama wengine ndani ya Hifadhi ya Taufa ya Serengeti.
Fisi wakijipoza joto na maji yaliyotuama ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Nyati ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Ndege wa aina mbalimbali wanaopatikana ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Seerengeti.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 

SHRIKA la Hifadhi za Taifa  (TANAPA) limeanza jitihada kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Mashirika makubwa ya ndege ,kuona ni namna gani yanaweza kusaidia katika kuinua sekta ya utalii hapa nchini.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi na Hifadhi za taifa, ndege aina ya ATR namba 5H-PWE inatua katika uwanja wa ndege uliopo katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti huku ikiwa na abiria 45 kutoka nchini Afrika kusini waliofika kwa ajili ya Utalii.

Ndege hii mali ya kampuni ya Shirika la ndege la Precision Air imetua majira ya saa 11:40 juzi jioni ikiwa ni ishara ya uzinuzi rasmi wa safari za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi katika hifadhi ya Serengeti ambazo sasa zitafanyika mara tatu kwa juma.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) Pascal Shelutete anasema kuanza kwa safari za ndege katika hifadhi hii kutaongeza idadi ya watalii ambao kwa sasa watatumia muda mfupi kufika hifadhini.

Kwa upande wa kampuni zinazojishughulisha na
biashara ya utalii nchini hatua ya shirika la ndege la Precision Air kufanya safari za moja kwa moja hadi hifadhi ya Serengeti ina maana gani kwao.

Hatua hii ikalisukuma Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanapa ,sasa kuangalaia uwezekano wa kuendelea kutoa ushawishi kwa mashirika mengine ya ndege kufanya safari zao katika hifadhi zilizopo kusini mwa Tanzania.

Kuhusu usalama katika viwanja vya ndege vilivyoko
katika Hifadhi za taifa Shelutete ameyaondoa hofu mashirika ya ndege na kwamba viwanja vimekaguliwa na vina uwezo wa kupokea ndege mbalimbali.

Kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja hadi
katika hifadhi za taifa ni fursa nyingine kwa Tanapa na kampuni za Utalii nchini kwa kuongeza idadi ya wageni watakaotembelea vivuito vya utalii na kuongeza pato la taifa kupitia fedha za kigeni.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PRECISION AIR YAANZA SAFARI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.
PRECISION AIR YAANZA SAFARI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhan5KdkhnZO91ttCEMklSNeWuVG8R_5HXVcxYlXJ-hT6_b1TC-JrdxKaU89bnl4EVNZFCpoAY3eiM0gwHTdN8RfrzG8_Ob89KRyffG3se2ykr-9LRmY3zg1y_BPRZ37AjmGywjQtEtUo3_/s640/_MG_5316+%25281024x683%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhan5KdkhnZO91ttCEMklSNeWuVG8R_5HXVcxYlXJ-hT6_b1TC-JrdxKaU89bnl4EVNZFCpoAY3eiM0gwHTdN8RfrzG8_Ob89KRyffG3se2ykr-9LRmY3zg1y_BPRZ37AjmGywjQtEtUo3_/s72-c/_MG_5316+%25281024x683%2529.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/precision-air-yaanza-safari-katika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/precision-air-yaanza-safari-katika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy