Madaktari na wataalamu wengine wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Tanzania Australia Society na Rafik...
Madaktari
na wataalamu wengine wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na
Tanzania Australia Society na Rafiki Surgical Mission wakimfanyia
upasuaji mgonjwa wa kuvimba mishipa na misuli katika mguu wake wa kulia na
kupandikiza katika sehemu yenye uhutaji husika leo Novemba 24, 2016. Madaktari bingwa wa Muhimbili
wanaofanya upasuaji huo ni Dk. Ibrahimu Mkoma, Dk Edwin Mrema, Dk. John Tupa na
Dk Frank Muhamba ambaye anapitia mafunzo ya kuwa daktari bingwa wa upasuaji.
Mwingine ni daktari bingwa wa upasuaji, James Savundra na wataalamu wenzake
kutoka Australia.
MADAKTARI
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji kwa
kutumia darubini (microvascular surgery) wa kuhamisha misuli
na mishipa ya damu kutoka kwenye mguu kwenda sehemu nyingine chini ya mguu (free
gracilis muscle transfer).
Upasuaji
huu wa aina yake na ambao mara nyingi huchukua muda wa saa sita hadi saba una
lengo la kujenga uwezo kwa watalaamu wa ndani ili waendelee kutoa huduma za
ubingwa wa hali ya juu kwa Watanzania wengi zaidi na vilevile kupunguza kasi ya
kupeleka wagonjwa nje.
Mkuu
wa Idara ya Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambaye pia
ameshiriki upasuaji huo Dk Ibrahim Mkoma amesema upasuaji huo
unagharimu kiasi cha dola 40,000 za Marekani nchini Australia ikiwa ni gharama
ya upasuaji tu.
Lengo
kubwa la ushirikiano wa upasuaji huu ni wataalamu kutoka Australia kuwaachia
taaluma ya upasuaji huo madaktari MNH ili iweze kuendelea kufanya upasuaji huo
mbeleni.
Aidha
Dk Mkoma amesema kuwa kuanzia mwakani kutakuwa na utaratibu ambao utaanzishwa Chuo
Kikuu cha Tiba Muhimbili, wa taaluma maalumu ya kusomea upasuaji wa aina hiyo
ili kuweza kupata wataalamu zaidi kutoka nchini.
Amesema
hakuna chuo chochote Tanzania kinachotoa taaluma hiyo ya plastic surgery kwa
sasa.
Dk
Mkoma amesema MNH inajivunia kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Australia
akiwapo Daktari bingwa James Savundra ambaye ni Rais wa Madaktari
Bingwa wa upasuaji kutoka timu ya upasuaji nchini Australia.
Daktari
bingwa wa upasuaji kutoka Australia, Dk James Savundra amesema
upasuaji huo ni moja ya upasuaji ambao umekuwa ukifanyika kwa
gharama kubwa.
“Nchini
Australia mgonjwa mmoja hufanyiwa upasuaji kwa dola 130 za Marekani kwa dakika
moja hiyo ikiwa ni gharama za chumba cha upasuaji ambazo ni kwa ajili ya kuwalipa
madaktari wa upasuaji, madaktari wa usingizi, wauguzi na watalaamu wengine
waliohusuka katika upasuaji huo,” amesema Dk Savundra.
Amesema
gharama hiyo haijumuishi huduma nyingine ambazo mgonjwa huyo anatakiwa kupata
ikiwamo huduma ya wodini na kadhalika.
“Tumefanya
upasuaji huu kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka nchini Australia
kupitia mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Tanzania Australia Society na
Rafiki Surgical Mission,”amesema Dk. Mkoma.
Mpaka
sasa wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa aina hiyo Muhimbili ni watatu mbali na
sita waliofanyiwa upasuaji mbalimbali ukiwamo upasuaji wa shavu, nyonga, mkono
na ziwa.
Mapema
wiki hii, Muhimbili imeanza kambi maalumu ya upasuaji kwa wagonjwa wenye
kuhitaji upasuaji maalumu kwa kushirikiana na madaktari hao kutoka nchini
Australia.
Hospitali
ya Taifa Muhimbili iko kwenye mageuzi makubwa katika kuboresha huduma
mbalimbali ambapo Disemba mwaka huu inatarajia kuanza kutoa huduma za
upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watoto wanaozaliwa na matatizo ya
usikivu. Wakati huohuo Januari mwaka 2017 Hospitali hii inatarajia kuanza
kufanya upasuaji wa kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye matatizo hayo.
Daktari
Bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Edwin Mrema
akizungumza na waandishi wa habari Leo katika chumba cha upasuaji ambako
kumefanyika upasuaji huo.
Madaktari
na wataalamu wengine wakiendelea na upasuaji leo.
Daktari
bingwa wa upasuaji na Mkuu wa Idara ya Upasuaji, Ibrahimu Mkoma akizungumza na
waandishi wa habari leo katika hospitali ya Muhimbili.
Wataalamu
na madaktari wakiendelea na upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
COMMENTS