MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI UFUNGUZI WA MABWENI YA WANACHUO MKOANI MWANZA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wanafunzi na wazazi waliojitokeza wakati wa...







 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wanafunzi na wazazi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi ya pongeza mara baada ya zoezi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza kukamilika katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhashamu Flavian Kassala ,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.
                                     ................................................................ 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kujenga na kuimarisha ushirikiano na taasisi za kidini nchini ili kuhakikisha miradi ya kijamii inayotekelezwa na taasisi hizo inaleta
manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi  wa wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kabla  ufunguzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo cha Maafisa Tabibu yaliyojengwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Geita kwa gharama ya shilingi milioni 659.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa  unaotolewa na taasisi za kidini nchini unaolenga kuimarisha utoaji wa huduma bora za kijamii na hivyo Serikali inaendelea kudumisha mahusiano mema yaliyopo kati ya Serikali na taasisi hizo za kidini nchini.

Makamu wa Rais pia amehimiza taasisi za kidini nchini kutumia vizuri misamaha ya kodi wanayopewa na Serikali ili kuhakikisha misamaha hiyo inakuwa na manufaa mazuri kwa jamii na sio vinginevyo.
Kuhusu uhifadhi wa chakula, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonya  vikali tabia ya baadhi ya wananchi kuuza mazao waliyovuna na baadaye kukabiliwa na uhaba wa chakula na kusema tabia hiyo sio nzuri na lazima ikomeshwe haraka iwezekanavyo.

Makamu wa Rais amewaagiza viongozi wa wilaya kote nchini kupambana ipasavyo na wimbi la uuzaji kiholela nafaka hasa nje ya nchini ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwa wananchi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI UFUNGUZI WA MABWENI YA WANACHUO MKOANI MWANZA
MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI UFUNGUZI WA MABWENI YA WANACHUO MKOANI MWANZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhA3PFgSVwYibWIhRIv2g9MPQnr5roibkwTIr-EML2VkA1Rm0XA_aEtGbNQ8u6UMZURlKyjcBRVZG0Ic3lEiXagT6VA6H-Y9h2goicJx8JUgcJ3r0Ve_NNOHYth5Gu4pvNscVbG0N46_fQ/s640/11.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhA3PFgSVwYibWIhRIv2g9MPQnr5roibkwTIr-EML2VkA1Rm0XA_aEtGbNQ8u6UMZURlKyjcBRVZG0Ic3lEiXagT6VA6H-Y9h2goicJx8JUgcJ3r0Ve_NNOHYth5Gu4pvNscVbG0N46_fQ/s72-c/11.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/makamu-wa-rais-samia-suluhu-hassan.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/makamu-wa-rais-samia-suluhu-hassan.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy