Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mery Majaliwa wakimsalimia Bahati Omary kutoka kijiji cha Nangao Wilaya Liwale ambaye ...
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mery Majaliwa wakimsalimia Bahati Omary
kutoka kijiji cha Nangao Wilaya Liwale ambaye amejifungua mtoto wa kike
katika Hospitali ya wilaya ya Nachingwea Waziri mkuu alifika katika
Hospitali hapo kujionea jinsi huduma za afya zinavyo tolewa kwa wagonjwa
waziri mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na
Ruwangwa Mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na watumishi wa Hospitali ya Nachingwea
pamoja na wananchi waliofika katika Hospitali ya nachingwea Waziri Mkuu
alifanya ziara ya kutembelea hospitalini hapo kwa ajili yakuona na
kusikiliza wagonjwa wanavyo pata huduma.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah
Chiwanga ambaye nimiongoni wa viongozi wa mkoa wa Lindi waliofika katika
kiwanja cha ndege Nachingwea kumpokea Waziri mkuu na mkewe Mary
Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ambao
wamewasili katika Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya
Nachingwea na Ruwangwa.
(Picha na Chris Mfinanga)
(Picha na Chris Mfinanga)
Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati alipotembelea
hospitali ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku
tatu mkoani Lindi.
Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaagiza taasisi zote za umma kutumia
mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kudhibiti
mianya ya upotevu wa fedha za umma.
Amesema taasisi ambazo tayari ziameanza kutumia mfuko huo
katika ukusanyaji wa mapato zimeweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. 300,000
hadi milioni nne kwa siku.
Pia aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha
wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao utawawezesha kupata
huduma ya matibabu bure katika kipindi cha mwaka mzima.
Akizungumzia kuhusu matibabu kwa wazee, Waziri Mkuu
amemuagiza Bw. Mohammed kuhakikisha anafungua dirisha la kuwahudumia wazee ili
kuwarahisishia upatikanaji wa huduma wanapofika hospitalini hapo.
“Mkurugenzi hakikisha watendaji wako wa kata na vijiji wamebaini
wazee wote katika maeneo yao na kuwatengenezea vitambulisho vitakavyowawezesha
kupatibiwa bure,” amesema.
Naye Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Samwel Laizer amesema
muamko mdogo wa jamii kujiunga na CHF ni moja kati ya changamoto zinazowakabili
katika utoaji wa huduma za afya.
Dk. Laizer amasema kati ya kaya 30,000 zilizoko wilayani
Nachingwea ni kaya 7,133 tu ndizo zilizojiunga na mfuko wa CHF.
Awali Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa wilaya hiyo
kwenye ukumbi wa Chuo Cha Walimu na kuwataka wabadilike ili waweze kuwatumikia
wananchi kwa uadilifu bila ya kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.
Amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayeshindwa
kutekeleza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi. “Serikali haitaridhika kuona
wananchi wakizagaa kwenye ofisi za halmashauri hiyo bila ya kusikilizwa,”
amesema.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI,
OKTOBA 16, 2016
COMMENTS