Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk Haruni Kondo. Mjumbe wa Bodi, Stella Nghambi. Mjumbe wa...
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk Haruni Kondo.
Mjumbe wa Bodi, Stella Nghambi.
Mjumbe wa Bodi, Dk Jasson Kagonza.
Mjumbe wa Bodi, Khadija Shaaban.
Mjumbe wa Bodi, Fatuma Bakari.
Mjumbe wa Bodi, Leonard Kitoka.
Mjumbe wa Bodi, Dk Ubena John.
Katibu wa Bodi ya Shirika la Posta, Rochus Assenga.
Kaimu
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga,
akizungumza kuhusu shirika hilo, kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa
Bodi, Dk Haruni Kondo, kuzungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya
shirika hilo jijini Dar es Salaam Oktoba 26 2016. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com )
Kaimu
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta, Fortunatus Kapinga, akizungumza
kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya shirika, Dk Haruni Kondo.
Mameneja wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya shirika hilo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi mpya ya Shirika hilo, wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi mpya wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Meneja
Mkazi Zanzibar wa shirika la Posta, Mwanaisha Saidi (katikati), Meneja
wa Huduma za Barua, Fadya Zam (kulia) na Meneja Utumishi wa shirika,
William Makumba (kushoto), wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta wakiwa katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika hilo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk Haruni Kondo, akitoa maelezo
mafupi kuhusu bodi hiyo mpya pamoja na shirika hilo kwa jumla kwa Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa,
kabla waziri Mbarawa hajaizindua rasmi bodi hiyo. Kushoto Ni Katibu Mkuu
wa wizara hiyo (Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Mawasiliano),
Profesa Faustine Kamuzora, akitoa hutuba yake kabla ya kumkaribisha
Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa, kutoa hotuba
yake ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania, jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta wakinukuu hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
wakati alipoizindua rasmi bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania, leo
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk Haruni
Kondo.
Baadhi
ya wajumbe wa bodi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipokuwa akitoa hotuba
yake ya uzinduzi wa bodi hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
wakati akiizindua rasmi bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania, leo
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk Haruni
Kondo.
Kaimu
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta, Fortunatus Kapinga (kushoto),
akifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya shirika hilo, leo
jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati),
akikata utepe mkoba wa vitendea kazi kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa
Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk Haruni Kondo (kulia), wakati wa
uzinduzi wa bodi hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, (Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati),
akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta
Tanzania, Dk. Haruni Kondo.
Mjumbe wa Bodi, Stella Nghambi, akitoa neno la shukurani baada ya Waziri Profesa Mbarawa kuizindua bodi hiyo.
Picha
ya Pamoja ya Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati
waliokaa), mara baada ya kuizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha
ya Pamoja ya viongozi wa Shirika la Posta na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto waliokaa), mara
baada ya kuizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
HOTUBA
YA MHESHIMIWA PROFESA MAKAME MBARAWA (MB) WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA
MAWASILIANO WAKATI WA UZINDUZI WA BODI MPYA YA SHIRIKA LA POSTA
TANZANIA,TAREHE 20 OKTOBA, 2016, KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO, GHOROFA YA
12, POSTA HOUSE MAKAO MAKUU.
· Katibu Mkuu wa Mawasiliano,
· Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania,
· Wakurugenzi wa Bodi,
· Kaimu Postamasta Mkuu,
· Viongozi wa Menejimenti,
· Wageni waalikwa,
· Mabibi na Mabwana,
· PONGEZI NA SHUKRANI
Awali
ya yote napenda nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa
rehema kwa kutujalia uhai na afya njema ya kuweza kujumuika hapa leo na
kushiriki katika uzinduzi huu wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la
Posta Tanzania.
Pia nawapongeza Wajumbe wote wa Bodi na Mwenyekiti kwa kuteuliwa kuongoza Shirika hili.
Ninawashukuru
kwa kunikaribisha ili niungane na kuzungumza nanyi wakati huu wa
kuzindua Bodi mpya. Fursa hii ni adimu kwani imetuwezesha kufahamiana
pamoja na kutafakari kwa kina juu ya changamoto zilizopo na kuanza
kubuni njia ya kuzitatua.
· MAJUKUMU NA CHANGAMOTO ZA SHIRIKA
Mwenyekiti wa Bodi,
Leo
hii nitawakabidhi baadhi ya nyenzo na nyaraka za majukumu ya Shirika na
Bodi ya Wakurugenzi kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Bunge Na. 19
ya mwaka 1993.
Sina
haja ya kutaja majukumu haya lakini ni vyema kuanzia sasa mzingatie
kuwa mawasiliano haya kwa njia ya Posta ni kichocheo na kielelezo
muhimu cha ukuaji wa uchumi wa Taifa lolote duniani.
Kwa
bahati nzuri Wajumbe wa Bodi hii ni wataalamu wenye uzoefu na
waliobobea katika nyanja muhimu ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wa
biashara, usimamizi wa rasilimali watu na rasiliamali fedha, sheria,
TEHAMA, ubunifu katika biashara, usalama na uendeshaji wa sekta binafsi.
· HALI YA HUDUMA ZA POSTA KITAIFA NA KIMATAIFA
Mwenyekiti wa Bodi,
Kwa
mujibu wa takwimu za Umoja wa Posta Duniani (UPU), mtandao wa
mawasiliano kwa njia ya Posta unajumuisha Ofisi za Posta laki sita na
sitini elfu (660,000).
Huu
ni mtandao mkubwa zaidi duniani ambao pamoja na huduma nyingine una
uwezo wa kusambaza wastani wa barua zipatazo 450 bilioni na vifurushi 6
bilioni kwa mwaka.
Hapa
Tanzania Shirika hili linaendesha mtandao wa Ofisi za Posta zipatazo
400. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo wastani watu 120,000 katika Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania wanahudumiwa na ofisi moja ya Posta. Kuhusu
ufikishaji barua na vifurushi katika ofisi na makazi ya watu (physical delivery of mail) kiwango
ni kidogo sana. Wastani wa 98% ya barua zinazohudumiwa na Shirika hili
hupitia katika masanduku ya barua yalioko katika ofisi za Posta.
Kiwango
hicho kinaonyesha wazi kuwa tunalo jukumu la msingi la kupanua na
kuboresha mtandao wa huduma za Posta hapa nchini ili kufikisha huduma za
kisasa za kimtandao karibu na jamii. Ningependa kusisitiza hapa kuwa
ni lazima Shirika hili liongeze kasi zaidi katika kuboresha na kuanzisha
huduma zinazozingatia matakwa ya wateja.
· SERA YA TAIFA YA POSTA
Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Kwa
hivi sasa Wizara yangu inaendelea kuhuisha Sera ya Taifa ya Posta ili
kuzingatia mahitaji ya sasa na baadae. Utekelezaji wa sera hii ni eneo
mojawapo ambalo inabidi tulizingatie.
Mwelekeo wa sera hii kwa muhtasari ni:-
· Kuwezesha Shirika la Posta ambalo ni mtoa huduma kwa umma (Public Operator) kutoa na kufikisha huduma bora kwa jamii yote na kwa gharama nafuu.
· Kuliendesha Shirika la Posta kwa misingi ya kibiashara.
· Kuzifanya
huduma za Posta kuwa za kisasa zaidi kwa kutumia teknolojia maridhawa
ili kukidhi mahitaji mapya ya wateja ambayo yanabadilika mara kwa mara.
· Kushirikisha
sekta binafsi katika kuendesha na kuwezesha shughuli za Posta ili
kuchochea maendeleo ya sekta hiyo na sekta nyingine kama za fedha,
biashara, afya, elimu, habari n.k
· Wizara
yangu inapenda kuona utekelezaji wa masuala yaliyoainishwa katika sera
ya Posta na kuhakikisha uhuishwaji wa sera hii ambayo ni ya muda mrefu
2003 ili kuwezesha malengo yanafikiwa.
· MATUMIZI SAHIHI YA FURSA NA RASILIMALI ZA SHIRIKA
Kwa
bahati nzuri Shirika la Posta ni moja ya Taasisi zenye rasilimali na
fursa nyingi ambazo kama zikitumiwa vizuri zinaweza kusaidia
kuliendeleza Shirika. Rasilimali na fursa hizo ni pamoja na:-
· Viwanja
na majengo ya kuishi na ya ofisi ambayo yako sehemu mbalimbali hapa
nchini na hasa yaliyopo maeneo ya mijini. Kwa mfano, Shirika lina
viwanja 178 na kati ya hivyo viwanja 153 vimeendelezwa na 25
havijaendelezwa.
· Mtandao
mpana wa ofisi za Posta zipatazo 400 hapa nchini ambao umeunganishwa
katika ofisi za Posta zipatazo 660,000 duniani kote (Global Connectivity).
· Uwezo mkubwa wa kutoa huduma unganishi za kimtandao (Integration of physical and digital solutions).
· Uwezo
mkubwa wa kuboresha huduma na biashara zilizopo na hapo hapo kuanzisha
mpya . Kwa bahati nzuri hata Sheria iliyoanzisha Shirika hili
inasisitiza juu ya jambo hili.
· Mna uwezo wa kurejesha imani kubwa ya kihistoria (Historical Loyalty) waliyonayo wateja na wadau mbalimbali wa Posta.
Naamini
mnafahamu kuwa mkakati huu wa kutumia vizuri fursa na rasilimali kama
hizi umefanywa na mashirika mengi ya Posta hapa duniani na umeyawezesha
mashirika hayo kuwa na mafanikio makubwa. Hali ni hivyo hivyo hapa
nchini kwani, baadhi ya mashirikia kama hili la Posta yametumia vizuri
fursa na rasilimali zilizopo na kuweza kufanikiwa.
Jambo
la msingi ni kuangalia maeneo yote hasa sheria zenye ukiritimba
zinazozuia Shirika kutumia rasilimali zake kwa ajili ya uzalishaji
mfano, sheria ya Shirika kuwa chini ya uangalizi wa Consolidated Holding
Corporation (CHC) ambapo haliwezi kukopa au kuweka rehani vitega
uchumi vyake ili kuendeleza huduma na biashara.
· MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI NA SIMBO ZA POSTA
Mwenyekiti na Wajumbe,
Anuani za makazi na simbo za posta (Physical Address and Post code System) ni
moja ya mradi mkubwa wa kitaifa ambao mwezi Septemba mwaka huu Waziri
Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alizindua muongozo wake mkoani Dodoma.
Aidha,
kuwepo kwa anuani zinazotambulisha makazi ya watu na rasimali za kudumu
kutatoa fursa nyingi zaidi katika utoaji na uendeshaji wa huduma za
posta nchini.
Ingawa
wadau wa utekelezaji wa mfumo huu ni wengi lakini Wizara yangu na
taasisi zilizoko chini yake hususani Shirika hili la Posta, Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) zina
wajibu mkubwa zaidi katika kuhakikisha manufaa ya mfumo huu yanawafikia
watumiaji wa mwisho ambao ni pamoja na wananchi wa kawaida (last mile Users). Manufaa hayo ni pamoja na:-
· Kuwezesha huduma za usambazaji na logistiks. Hili ni eneo linalopanuka kwa haraka sana hapa nchini na duniani kote.
· Kuwezesha huduma jumuishi za kimtandao hususani za biashara (E-business), elimu (E-education), afya (E–medicine), utawala serikalini (E – governance) na nyinginezo.
· Uboreshaji
wa huduma za dharura na usalama kama zima moto na uokoaji, polisi,
magari ya wagonjwa, majanga kama matetemeko, mafuriko na vimbunga.
· Kurahisisha usajili wa huduma, biashara, na mifumo mbalimbali kama vizazi, vifo, ndoa na talaka.
· Kukuza utalii wa ndani na nje pamoja na kurahisisha utambuzi wa sehemu kwa wageni.
· Kuboresha utendaji wa taasisi nyingine kama za Ugavi wa Nishati na Maji, Mabenki, Mamlaka za mapato, Bima na Hifadhi ya Jamii.
Kwahiyo
lazima tuzingatie kuwa watu wote na taasisi zote hizo zinatutegemea
katika kufanikisha mfumo huu wa Anuani za Makazi na Postikodi.
Tafadhali tusiwaangushe.
7.0 HUDUMA YA POSTA MLANGONI
Mwenyekiti na Wajumbe,
Kwa kuzingatia mwelekeo huu, Shirika hili limeanzisha huduma mpya ijulikanayo kama “POSTA MLANGONI”. Huduma hii tajwa imeanzishwa hapa Dar es Salaam, Dodoma na Arusha.
Ni
mwanzo mzuri, lakini ningependa mwongeze jitihada katika jambo hili.
Mwelekeo wetu uwe ni kuzingatia maslahi mapana ambayo ni pamoja na:-
· Kujenga nchi ya viwanda.
· Kufikiwa malengo ya Dira ya Taifa ya mwaka 2025 (Vision 2025).
· Kupunguza umaskini na kurahisisha utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii.
8.0 UTEKELEZAJI WA MIUNDOMBINU MINGINE
Mwenyekiti na Wajumbe,
Pamoja
na utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi na Postikodi ili
kufanikisha dhamira yetu ya kitaifa, kwa bahati nzuri nchi yetu imefikia
hatua ya kuridhisha katika kusimika miundombinu mingine muhimu ya
kufanikisha dhamira hii.
Miundombinu hii ni pamoja na:-
· Upanuzi wa Mkongo wa Taifa na Ujenzi wa mikongo ya mijini (Metro fiber network).
· Ujenzi wa kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (Data – Centre).
· Uboreshaji wa mtandao wa barabara, viwanja vya ndege na bandari.
· Usambazaji wa huduma za nishati ya umeme katika maeneo yote ya nchi yetu.
Nawaagiza Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti, na Wafanyakazi wote wa
Shirika hili changamkieni fursa za miundombinu hii.
9.0 HITIMISHO
Mwenyekiti,
Kabla ya kumaliza hotuba yangu ningependa kusisitiza juu ya maeneo yafuatayo:-
· Uwajibikaji, uchapakazi na ubadilishwaji wa mtazamo (change of mind sets) ya wafanyakazi wa Shirika hili. Tuondokane na kuendesha shughuli zetu kwa mazoea (business as usual). Hii ni pamoja na kuwajengea uwezo katika teknolojia ya kisasa.
· Kuongeza
udhibiti wa usalama katika mtandao wa Shirika. Tuwe macho na uhalifu
wa kimtandao kama usafirishaji wa madawa ya kulevya, utakatishaji wa
fedha na uzingatiaji wa jumla wa sheria za nchi na Kimataifa.
· Kuanzisha huduma ya “One Stop Community Centre”. Hii iende sambamba na kuimarisha huduma za uwakala kwa kutumia TEHAMA ikiwa ni pamoja na kuwa na “Payment Switch”.
· Eneo lingine ni kutoa huduma bora zinazowaridhisha wateja (customer satisfaction). Hii ni pamoja na kuimarisha shughuli zenu za masoko.
· Kupanua wigo wa biashara, kuongeza mapato, kupata faida na hatimaye kutoa gawiwo kwa mwenye hisa ambaye ni serikali.
Nafahamu
baadhi ya mambo haya yako katika mipango yenu ila la muhimu ni
ufuatiliaji na utekelezaji wenu. Kwa upande wa Serikali tunatambua na
kuzingatia changamoto za msingi za Shirika hili ikiwa ni pamoja na
ukosefu wa mtaji na mzigo wa kulipa pensheni za wastaafu wa Jumuiya ya
zamani ya Afrika Mashariki.
Baada ya kuyasema hayo, sasa natamka kuwa – Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania, IMEZINDULIWA RASMI.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
COMMENTS