Wakulima wakipalilia mashamba yao ya mizabibu mkoani Dodoma. Mche wa mzabibu shambani kabla ya mavuno. ...
Wakulima wakipalilia mashamba yao ya mizabibu mkoani Dodoma.
Mche wa mzabibu shambani kabla ya mavuno.
“Kwa muda mrefu
wakulima wa zabibu mkoani Dodoma tumekuwa tukikabiliwa na changamoto mbalimbali
kiasi kwamba licha ya kufanya kazi za kilimo hususani cha mazao ya biashara
tumekuwa tukiendelea kukabiliwa na tatizo la kutopata faida na kubaki katika
hali duni za kutuwezesha kupata mahitaji muhimu ya kukidhi mahitaji yetu
ikiwemo kujenga nyumba bora na kusomesha watoto wetu”Anasema Yarendi Makuya, mkulima wa zabibu kijiji cha Handala
mkoani Dodoma.
Anasema kuwa katika miaka ya
karibuni kutokana na kuongezeka kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda wakulima
wa zabibu wameanza kupata ahueni ya maisha kutokana na wateja wanaowatembelea
vijijini wakihitaji kununua zao la
zabibu wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku hali inayotia matumaini kuwa kilimo
cha zao hilo kina fursa ya kuchangia uchumi na kuinua maisha ya wakulima iwapo
watawezeshwa ipasavyo.
Yarendi aliyekuwa akiongea kwa niaba ya wenzake alieleza kuwa hivi
sasa baadhi ya makampuni yaliyowekeza kwenye viwanda yameanza kujenga ukaribu na kushirikiana na
wakulima ili yaweze kupata malighafi kwa ajili ya viwanda vyao na kuhakikisha
uzalishaji wa zao hili unaongezeka.
Moja ya kampuni aliyoitaja
kuwa hivi sasa imejikita katika kilimo
shirikishi na wakulima wa zabibu na ushirikiano huo umeanza kuonyesha mafanikio
ni kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama Konyagi iliyopo
chini ya TBL Group ambayo hivi sasa inashirikiana na wakulima kwa lengo la
kuwawezesha kuongeza uzalishaji wa
zabibu kupitia mpango wa Go Farming na
wakati wa msimu inanunua zao hilo kwa bei nzuri na malipo kufanyika bila
urasimu kama ilivyokuwa hapo awali walipokuwa wanauza zabibu kupitia vituo vya
Ushirika na walanguzi wa mazao ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa
wakiwapunja katika bei ya kuuzia.
COMMENTS