Kamishina Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah akizungumza katika hafla ya kukabidhi kukabidhi nyaraka za...
Kamishina
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah akizungumza katika
hafla ya kukabidhi kukabidhi nyaraka za kutagaza Utalii kwa ujumbe wa
skauti utakaokwenda Korea Kusini.
Kaimu
Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga
(kushoto) akimkabidhi nyaraka za kutangaza utalii Mskauti Mkuu, Mwantumu
Mahiza ambaye ataongoza ujumbe wa chama cha skauti Tanzania huko Korea
ya Kusini. Kulia ni Kamishina Mkuu wa Skauti, Abdulkarim Shah.
Mskauti
Mkuu, Mwantumu Mahiza ambaye ataongoza ujumbe wa chama cha skauti
Tanzania huko Korea ya Kusini akizungumza katika hafla hiyo.
Stakauti wakiimba nyimbo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga (kushoto)
akimkabidhi nyaraka za kutangaza utalii pamoja na bendera ya Taifa Mskauti
Mkuu, Mwantumu Mahiza ambaye ataongoza ujumbe wa chama cha skauti cha Tanzania huko
Korea ya Kusini. Kulia ni Kamishina Mkuu wa Skauti, Abdulkarim Shah.
TAARIFA
FUPI YA KAMISHNA MKUU WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA ILIYOTOLEWA TAREHE
27/07/2016 KWENYE HAFLA FUPI ILIYOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA MAKAO MAKUU YA
CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA UPANGA YA KUUKABIDHI UJUMBE WA CHAMA CHA SKAUTI
TANZANIA NYARAKA ZA KUTANGAZA UTALII WATAKAPOKUWA SAFARINI HUKO KOREA YA KUSINI
Viongozi wetu wote wa juu wa nchi hii kwa vipindi tofauti wamekuwa wakizungumzia maisha bora kwa wananchi wake.
Rais wetu wa awamu ya tano, Mhe. John Pombe Magufuli hali kadhalika
anazungumzia maisha bora na yenye neema kwa raia wake. Ametuambia mara nyingi
anataka kuigeuza nchi yetu kuwa ya viwanda vitakavyoongeza ajira kwa vijana na
hatimae nchi yetu iweze kuwa miongoni mwa nchi wahisani. Hii ndio ndoto ya Rais
wetu wa awamu ya tano.
Chama cha Skauti Tanzania kina dhima
ya malezi ya watoto na vijana. Malengo makuu ya Chama hiki ni kuwaendeleza
watoto na vijana kimwili, kiakili, kihisia, kijamii na kiroho na wakati huo
watoto na vijana hawa wawe raia wema na wazalendo wa kweli wa nchi hii wenye
manufaa kwa Taifa lao na watu wake.
Chama cha Skauti Tanzania kinatekeleza
dhima yake kwa dhamira kubwa na ya kweli. Chama kinalea watoto na vijana ambao
hatimae wanakua wenye afya bora, jasiri na wenye uthubutu. Vijana hawa wanaweza
kuaminika katika utumishi wa umma na hata sekta binafsi.
Wanaweza kulitumikia
Taifa lao kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa uzalendo wa hali ya
juu, kwenye Wizara na idara za Serikali Kuu na za Mitaa, mashirika ya Umma na
Sekta binafsi kwa uaminifu mkubwa. Aidha sifa moja kubwa walionayo vijana hawa
ni kujituma katika shughuli za kijamii kwa njia ya kujitolea.
Vijana wetu
tuliowaandaa wana mchango mkubwa sana katika kuifikisha jamii kwenye ndoto za
viongozi wetu wa nchi. Tuwape nafasi na
tuwatume na watatumika bila kinyongo na watatoa matokeo chanya tarajiwa.
COMMENTS