KAMPUNI YA TING YATOA MAGETI YA CHUMA KUDHIBITI WEZI WA KOKI ZA MAJI UWANJA WA TAIFA

Naibu Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura (wane kushoto), akipeana mikono na Mkurugenzi Mtend...








Naibu Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura (wane kushoto), akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ting, Father Fernandez, wakati akipokea msaada wa mageti kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Juni 17, 2016. Kampuni hiyo imetoa mageti 27 yenye thamani ya shilingi Milioni 44.







NA
K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
KAMPUNI ya kusambaza ving'amuzi vya televisheni ya Ting ya jijini Darves Salaam, imekabidhi mageti ya chuma  27 kwa
uongozi wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ili kuwadhibiti “wakora” wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki za maji.
Akipokea msaada huo leo Juni 17, 2016 kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanjanin hapo, Naibu Waziri wa Habri, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura, ameishukuru
kampuni hiyo kwa msaada huo ambao utakomesha vitendo vya wizi na uharibifu wa miundo mbinu ya uwanja huo wa soka wa kisasa kabisa hapa nchini
“Mwanzoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu, nilifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huu na kujionea uharibifu mkubwa kwenye vyoo ambapo koki za maji
zimeibiwa na hivyo kusababisha baadhi ya vyoo kufungwa na kupelekea usumbufu mkubwa kwa mashambiki was ok.” Alisema Naibu Waziri.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ting, Mchungaji Dkt. Veron Fernandes, alisema kampuni yake ambayo inajishughulisha na uagizaji na usambazaji wa ving’amuzi, imeona inao
wajibu mkubwa wa kusaidia sekta ya michezo kwenye eneo hilo la kutunza miundombinu ya uwanja wa Taifa.
Alisema, Ting imetoa jumla ya mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44 ambayo yatasaidia kudhibiti wezi wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki na kuharibu miundombinu mingine.
K-VIS
MEDIA imeshuhudia koki za maji kwenye baadhi ya vyoo zikiwa zimeng’olewa.


 Mkurugenzi wa kampuni ya Ting, Mchungaji Dkt.Vernon Fernades, akimuonyesha moja ya mageti hayo Naibu Waziri Anastazia James Wambura
 Mkazi wa jijini Dar es Salaam, akitoka kwenye vyoo vya juu vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambavyo vimeathirika sana na wizi huo, Mageti hayo yatafungwa kwenye vyoo hivyo vya juu uwanja mzima
 Mkazi wa jiji akijisaidia kwenye moja ya vyoo hivo huku upande wa kushoto bomba linaonekana likiwa limeng'olewa koki.
 Naibu Waziri akizungumza wakati wa makabidhiano hayo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkenyenge
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkenyenge, (kushoto), akizungumza mbele ya Naibu Waziri, Wambura (katikati) na Mkurugenzi wa Ting, Dkt. Fernados
 Naibu Waziri akizungumza na Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa, Julius Mgaya, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo.
 Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa, Julius Mgaya (katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ting, Dkt. Fernandes, wakimpokea Naibu Waziri
 Naibu Waziri akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ting, Dkt. Fernandes, wakati akiwasili uwanja wa Taifa kupokea mageti hayo
 Sehemu ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambao baadhi ya watu wamekuwa wakihujumu miundombinu yake
 Wafanyakazi wa kampuni ya Ting
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ting, akiwa na baadhi wa wafanyakazi na wawakilishi wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara
Nyasi za uwanja wa Taifa zikipunguzwa kwa mashine maalum

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMPUNI YA TING YATOA MAGETI YA CHUMA KUDHIBITI WEZI WA KOKI ZA MAJI UWANJA WA TAIFA
KAMPUNI YA TING YATOA MAGETI YA CHUMA KUDHIBITI WEZI WA KOKI ZA MAJI UWANJA WA TAIFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEic65OALwU6tQjkOOfQpjoPKE-I6VX0f8Db-Yjjz5qrf8Z9ILLWKXPDDFmwZpjwVT-iF1oevhOeKLT199NPKtTcN2ZTRpmgTQ4fEYs-ZcSrJXQvOIR1mmgw13j3Cj1-3sutgbCsjEYFrT4/s640/3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEic65OALwU6tQjkOOfQpjoPKE-I6VX0f8Db-Yjjz5qrf8Z9ILLWKXPDDFmwZpjwVT-iF1oevhOeKLT199NPKtTcN2ZTRpmgTQ4fEYs-ZcSrJXQvOIR1mmgw13j3Cj1-3sutgbCsjEYFrT4/s72-c/3.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/06/kampuni-ya-ting-yatoa-mageti-ya-chuma.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/06/kampuni-ya-ting-yatoa-mageti-ya-chuma.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy