Aliyekuwa Mbunge Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), amelalamikia kuhujumiwa baada ya ofisi zake kwa nyakati tofauti kuvunjwa na kisha k...
Aliyekuwa Mbunge Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), amelalamikia kuhujumiwa baada ya ofisi zake kwa nyakati tofauti kuvunjwa na kisha kumwibia nyaraka mbalimbali na mali za thamani kubwa.
Matukio hayo yamefanyika kwa nyakati tofauti ambapo Machi 5, mwaka huu watu wasiojulikana walivunja ofisi yake iliyoko Posta katikati ya Jiji la Dar es Salaam waliiba vitu mbalimbali wakati tukio kama hilo lilirudiwa Machi 13 katika ofisi yake ya Chang'ombe ambapo zilichukuliwa nyaraka za uchaguzi wa mwaka jana pekee licha ya kuwa kulikuwa na vitu vingine vya thamani kubwa.
Hali kadhalika usiku wa kuamkia Juni, 26 (leo) wezi hao wameingia tena katika ofisi hiyo baada ya kufanikiwa kumpa mlinzi chakula kinachodaiwa kuwekwa dawa za kulevya ambapo alilala ndipo walipata mwanya wa kuiba pikipiki tatu zilizokuwa zimehifadhiwa katika ofisi hiyo, viroba vitatu vya mchele na boksi tano za tende.
Abbas Kilapo (aliye vaa kofia) akiwaonyesha Askari kanzu wa Kituo cha Chang'ombe jinsi watu hao walivyofanikiwa kwa kuondoka na vitu hivyo.
Muhusika wa ofisi hiyo ambaye alifahamika kwa jina la, Abbas Kilapo akiwaonyesha Askari Kanzu na waandishi wa hapari (pichani hawapo) Namba za pikipiki na kadi za Pikipiki zilizo ibiwa na watu wanaodaiwa ni wezi.
Abbas Kilapo akizungumza na waandishi wa habari (pichani hawapo) mara baada ya kufika Ofisini hapo.
Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Miburani, Ally Kamtande akimpepea inzi mlinzi huyo anayesadikiwa kupewa chakula chenye kilevi na kulala bila kujitambua Dar es Salaam jana. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA
COMMENTS