KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AWAPA MATUMAINI WATUMISHI 597 WA NIDA WALIOSITISHWA MIKATABA YAO

Afisa Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jemima Mulokozi (kushoto) akimuonyesha...



Afisa Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jemima Mulokozi (kushoto) akimuonyesha vitambulisho vilivyokamilika vikiwa na ubora unaohitajika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 28, 2016. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
 
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ansigar Chilemba akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam
NA FELIX MWAGARA, MOHA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.
Rwegasira alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya Watumishi hao waliachishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka mishahara ya miezi mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makato ya fedha za Bima ya Afya.
Akuzungumza na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa Vitambulisho vya Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka watumishi hao waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote kuhusu kutokulipwa haki zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha taratibu ndogo ndogo  kabla ya kuanza kuwalipa.
“Naomba muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani Serikali ipo makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo taratibu ndogo ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.
Aidha, Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23 wanatakiwa watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa Vitambulisho vya Taifa.
Hata hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya utambuzi  itakamilika kama ilivyopangwa na itafanyika kwa umakini mkubwa kama inavyotarajiwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha kazi pamoja na kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
“Tunakuahidi Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya kazi kadiri ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’, alisema Dk. Kipilimba
Katibu Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) akimsalimia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, wakati alipokuwa anawasili katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi. 


WANAFUNZI wa Stashahada ya Ualimu, Sayansi, Hisabati na Teknolojia, Chuo Kikuu Cha Dodomd (UDOM), wamerudishwa nyumbani na ifikapo Leo saa 12 jioni MEI 29, 2016, wanafunzi wote tajwa wanatakiwa wawe wameondoka kwenye mazingira ya chuo.  Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na ofisi ya makamu MKUU wa chuo hicho kikubwa kabisa hapa nchini ambacho huchukua watoto wengi wa makabwela Jumamosi MEI 28, 2016, inesema ni utekelezaji wa agizo la Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, ambapo baada ya kubaini matatizo ya ufundishaji duni wa taaluma tajwa, wizara iliagiza wanafunzi wanaochukua masomo hayo warejee nyumbani mara moja na serikali itawajulisha mustakbali wa masomo yao haraka iwezekanavyo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AWAPA MATUMAINI WATUMISHI 597 WA NIDA WALIOSITISHWA MIKATABA YAO
KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AWAPA MATUMAINI WATUMISHI 597 WA NIDA WALIOSITISHWA MIKATABA YAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSA1tiaRx_Y3cyFRGUxIWse7SFTj-sxWqocOK-GV4-2ImiZDj01kip0g8FJkL5imxSVA-lhNvCGgd4lY-OuLS2T6LE3ozvpjEP5Jv4A7FS5U0DxtX1MpBI8-R7AmrKzOu2xD3HkfONYls/s640/PIX+4.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSA1tiaRx_Y3cyFRGUxIWse7SFTj-sxWqocOK-GV4-2ImiZDj01kip0g8FJkL5imxSVA-lhNvCGgd4lY-OuLS2T6LE3ozvpjEP5Jv4A7FS5U0DxtX1MpBI8-R7AmrKzOu2xD3HkfONYls/s72-c/PIX+4.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/05/katibu-mkuu-mambo-ya-ndani-awapa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/05/katibu-mkuu-mambo-ya-ndani-awapa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy