KUTOKANA na ugeni wa ujio wa mabasi ya mwendao kasi UDART ambayo yanamfumo wake wa barabara, palitarajiwa kutokea ma...
KUTOKANA na ugeni wa ujio wa mabasi ya mwendao kasi UDART ambayo yanamfumo wake wa barabara, palitarajiwa kutokea matukio ya watu kugongwa kutokana na kujengeka kwa tabia ya watu kuvuka bila kuzingatia alama za kuvukia. Leo hii Mei 19, 2016, pametokea tukio la kusikitisha ambapo mwanafunzi wa darasa la pili kwenye shule moja ya msingi aliyetambuliwa kwa jina la Nasra Mkinze, amepoteza maisha baada ya basi lenye namba T953 DGV kumgonga mpanda bodaboda aliyekuwa amembeba mtoto huyo na shemeji ya mpanda bodaboda kwenye taa za kuongozea magari Shekilango Ubungo jijini Dar es Salaam.
Bodaboda iliyozua balaa ikiwa mikononi mwa polisi wa usalama barabarani. (Picha na Khamisi Mussa)
COMMENTS