MHANDISI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA MAJIPU

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo kw...








 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo kwa kufanyakazi chini ya kiwango pamoja na wasaidiziwake wawili.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo, Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango. Kulia ni Msaidizi wa Meya, Semmy Mbegha.
Na Dotto Mwaibale

MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imemvua madaraka Mkuu wa Idara ya ujenzi, Mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko aliwataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajari Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi unaoendelea.

Kuyeko alisema  kikao cha Baraza la Madiwani kimefikia uamuzi huo baada ya manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa barabara mbovu ndani ya manispaa hiyo.

Alisema baada ya kuingia madarakani kwa miezi mitatu walijaribu kutafuta kero ndani ya manispaa ya Ilala ambapo walibaini idara ya ujenzi ina malalamiko mengi kutoka kwa madiwani wa kata mbalimbali kwa sababu ya kusimamia ujenzi wa barabara chini ya kiwango na hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa na maofisa hao.

Alisema madiwani hao walimlalamikia Mhandisi Bwigane kuwa amekuwa akikaidi wito wao wa kujadili ujenzi wa barabara mbovu pindi zinapobainika jambo ambalo limesababisha manispaa hiyo kuwa na barabara nyingi mbovu.

Jitihada za gazeti hili za kumtafuta Mhandisi Bwigane ili kuzungumzia kusimamishwa kwake kazi hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu yake na wakati wote kuwa imefungwa.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MHANDISI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA MAJIPU
MHANDISI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA MAJIPU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgDAOnGmLwdxsOG9-ArOttQ_K-bluYRl_y0tObyID5VutXcDm26UDx8P0D2Rvys-SpU51l0SI5w1GT8gpgfYYBMIw5G-JuOst4mOHR3xbwDOYTHCnOhgxGtpPYiUIatSFhxSgNal4TpDqGi/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgDAOnGmLwdxsOG9-ArOttQ_K-bluYRl_y0tObyID5VutXcDm26UDx8P0D2Rvys-SpU51l0SI5w1GT8gpgfYYBMIw5G-JuOst4mOHR3xbwDOYTHCnOhgxGtpPYiUIatSFhxSgNal4TpDqGi/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/04/mhandisi-manispaa-ya-ilala-jijini-dar.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/04/mhandisi-manispaa-ya-ilala-jijini-dar.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy