Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi...
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri wasiorudisha fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni na fomu ya Ahadi ya Uadilifu wamesisitizwa kurudisha fomu hizo leo kabla ya saa 12 jioni katika ya Ofisi ya Tume ya Maadili iliyopo jijini Dar es salaam na watakaoshindwa kufanya hivyo watakua wamejitoa wenyewe kwenye nafasi zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majliwa ofisini kwake alipokutana na Waandishi wa Habari akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki, ambapo ameeleza kuwa, kufuatia Semina iliyofanyika Februari 25 mwaka huu kati yake na Mawaziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu, ambapo Kamishna Mkuu, Mhe. Jaji Mstaafu Salome Kaganda alitoa maelezo kwamba kuna baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao hawajarudisha fomu hizo hadi kufikia jana.
Akiwataja Viongzoi hao, Mhe. Majaliwa alisema kuwa, Mawaziri ambao hawajarudisha fomu hizo ni akiwemo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. January Makamba, ambao wote hawajarudisha fomu za Rasilimali na Madeni na fomu za Ahadi ya Uadilifu, vilevile Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga ambaye hajarudisha fomu ya Ahadi ya Uadilifu, na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, ambaye hajarudisha fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni, pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. Luhaga Mpina ambaye hajarudisha fomu zote mbili.
Mhe. Majaliwa, amewasisitiza Mawaziri hao kujaza fomu hizo kwa kua ni agizo la Mheshimwa Rais kujaza fomu hizo leo kabla ya saa 12 jioni, “viongozi watakaoshindwa kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni na fomu ya Ahadi ya Uadilifu wanatakiwa kujieleza kwa kutoa sababu za kushindwa kufanya hivyo na watachukuliwa hatua” alisema Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 9 Sheria ya Maadili ya Uongozi wa Umma ya mwaka 1995 sura ya 8 inawataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma (Tamko la Raslimali na Madeni) na fomu ya Ahadi ya Uadilifu mara wanapoteuliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi. Lengo la kujaza fomu hizo ni kuwa na uwajibikaji kwa kiongozi juu ya uadilifu wake wakati wote anapokua mtumishi wa Umma.
COMMENTS