Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua ujenzi wa Jego la Halmashauri ya Wilaya ya Peramiho akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Jan...
Waziri Mkuu, Kassim
Majliwa akikagua ujenzi wa Jego la Halmashauri ya Wilaya ya Peramiho akiwa
katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Januari 4, 2015. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
|
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amekagua jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wialaya ya Songea lilipo katika
kijiji cha Lundusi, Wilaya ya Peramiho mkoani Ruvuma.
Alipowasili jana katika eneo hilo alikutana na viongozi wa
jadi ambapo Mzee Daniel Gama alimkabidhi ngao na silaha ikiwa ni ishara ya kumkaribisha
kijijini hapo, pia alipata fursa ya kutazama ngoma ya mila ya kabila la
Wangoni.
Mara baada ya kukagua jengo
hilo la ghorofa,Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Lundusi Bwana Rajabu Mtiula amesema jengo hilo lenye ofisi 50, vyoo 4, ukumbi mkubwa 1 na kumbi
ndogo 2, ambapo mradi huo umetekelezwa kwa fedha za mfuko wa Mradi wa Maendeleo
na Serikali. Hadi sasa Serikali imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 200 na utekelezaji wake
umekamika kwa 85%, hivyo wanatarajia kuanza kutumia jengo hilo mwezi Februari,
2016.
Akizungumza jana (Jumatatu,
Januari 4, 2016) na wananchi wa kijiji
cha Lundusi, Waziri Mkuu, amewapongeza wananchi wa Lundusi kwa hatua hiyo ya maendeleo na
kusema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono ujenzi wa jengo hilo.
Waziri Mkuu Majaliwa,
ametaka kuwepo na mikakati ya uboreshaji wa eneo hilo kwa kusogeza huduma
karibu ili kuvutia watu zaidi katika eneo hilo.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu,
Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ametoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John
Magufuli na Waziri Mkuu kwa kuchaguliwa na kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano.
Pia, ameishukuru Serikali
kwa kusaidia kujenga jengo hilo, na pia ameeleza kero mbalimbali zinazowakabili
wananchi wa maeneo hayo ikiwemo wakulima kutofaidika kwa bei ya soko ya kuuza
mahindi, kutokuwepo na umeme na maji.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza
Waziri Jenista kufuatilia kero hizo kwa Wizara husika na baadae kuleta mrejesho
kwa wananchi.
Waziri Mkuu Majaliwa
anaendelea na ziara mkoani Ruvuma, leo siku ya jumanne (Januari 5, 2016) atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa na kuongea na Watumishi wa hospitali hiyo
na baadae ataongea na Watumishi wa Umma.
COMMENTS