Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishiriki na Wananchi, Vikundi ya vya usafi wa mazingira pamoja na Vikosi...
Balozi
Seif akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira Mwenyekiti wa Kikundi cha
Usafi wa Mazingira cha Kilimani { Kilimani City } Nd. Khamis Shaali
Chum { mwenye T. Shirt Nyeupe }vilivyotolewa zawadi na Ofisi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira.
Kushoto
ya Mwenyekiti huyo wa Kilimani City ni Mkurugenzi Maingira Nd. Juma
Bakari Alawi na wa kwanza kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka
ya Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja.
Picha na – OMPR – ZNZ.
NA Othman Khamis Ame, OMPR
Kazi
za usafi wa mazingira kwenye maeneo tofauti Nchini katika kuanza rasmi
kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
zimeonekana kuitikiwa vyema na Wananchi walio wengi pamoja na vikosi
vya ulinzi hapa Nchini.
Hali
ya mazingira salama katika mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi imeonekana
kubadilika kidogo kutokana na juhudi kubwa iliyofanywa na washiriki wa
zoezi hilo la usafi wa mazingira iliyoanza mapema asubuhi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alijumuika na Wananchi
hao kwa kazi za usafishaji wa Mtaro wa maji machafu unaokusanya maji
kutokea mitaa ya Muembe Njugu, Kwahani, Kariakoo, Kilimani na
Kumalizikia Pwani ya Kilimani.
Wapiganaji
wa Vikosi vya Mafunzo, Jeshi la Kujenga Uchumi, Kikosi Maalum cha
Kuzuia Magendo, Zimamoto na Uokozi, Valantia, vikundi vya usafi wa
mazingira vilivyomo ndani ya Wilaya ya Mjini, watendaji wa Baraza la
Manispaa na Wananchi walionekana kuhamasika katika harakati hizo.
COMMENTS