SHULE YA ST. JUDE ARUSHA, YAPONGEZWA Shule Direct ni taasis iinayoboresha fursa za mwanafunzi kuweza ku...
SHULE YA ST. JUDE ARUSHA, YAPONGEZWA
Shule
Direct ni taasis iinayoboresha fursa za mwanafunzi kuweza kusoma, kufanya mazoezi
na kujadiliana katika masomo mbalimbali na wanafunzi wenzake pamoja na walimu kwa
kutumiaTeknolojia. Elimu bora ni haki ya kila mtoto na kila mwanafunzi. Ukuaji
wa Teknolojia Tanzania na barani Afrika kwa ujumla unapaswa kuwa nyenzo ya
kuboresha upatikanaji wa maarifa na elimu ambapo kuna changamoto
nyingi zinazo wazuia wanafunzi kuipata. Shule Direct inaamini kwamba elimu inapaswa kupatikana saa yoyote na
mahali popote kwa sababu elimu ni chachu ya kubaini uwezo na vipaji vilivyomo ndani
ya mtu.
Shule ya Sekondari ya St. Jude kwa namna ya pekee wameelewa azma na
malengo ya Shule Direct. Hawakuwahi kuwaambia Shule Direct kwa maneno lakini takwimu
zinaelezea ukweli huu. Ni shule inayoongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi wanaojifunza
kupitia tovuti ya Shule Direct kuliko
Shule nyingine yoyote; na kufuatiwa na Shule ya Sekondari ya Wavulana ya
Azania na ya tatuni Shule ya Sekondari ya Kibasila. Wanafunzi wa shule
hizi wametumia muda mwingi zaidi kujifunza kupitia Shule Direct kuliko watumiaji
wengine. Shule hizi ni mfano wa kuigwa kwa sababu maarifa haya na mipaka, kadri
tunavyojenga hulka ya kutafuta na kujifunza kwa kutumia fursa mbalimbali, hivyo
ndivyo wanafunzi watakavyokuwa hata pale watakapokuwa wamemaliza shule. Kwa namna
ya pekee, Shule Direct wanawapongeza na kuwasifu shule ya St. Jude kwa sababu wamekuwa
mfano wa kuigwa.
Wanafunzi
walioongoza kujifunza kupitia Shule Direct kutoka Shule ya St. Jude, (kwa kutumia
majina yao ya kujisajili, (wala si majina yao kwa kweli), ni Boy, Brightstar,
Nasmar, Mkavi, Chrisspros, Mathew, Bob, Muller, Amaur, Shabbb, Jariss.j. jr.
Tunawazawadia wanafunzi hawa“digital coins” za Shule Direct zitakazowawezesha kununua
vitabu na vifaa mbalimbali kupitia hapo hapo kwenye tovuti.
(imeandaliwa na www.shuledirect.com)
COMMENTS