CCM MORO WAFAGILIA ZIARA ZA KINANA MIKOANI, NI KATIKA SEMINA YA VIONGOZI WA WAZAZI KINONDONI.

CCM MORO WAFAGILIA ZIARA ZA KINANA MIKOANI, NI KATIKA SEMINA YA VIONGOZI WA WAZAZI KINONDONI.   Mgeni rasmi, Dorothy Mwamsiku a...

CCM MORO WAFAGILIA ZIARA ZA KINANA MIKOANI, NI KATIKA SEMINA YA VIONGOZI WA WAZAZI KINONDONI.

  Mgeni rasmi, Dorothy Mwamsiku akiingia ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM Kinondoni, Charles Mgonja.

Mgeni rasmi akiwa na viongozi wa Jumuia ya Wazazi na CCM, baada ya kuingia ukumbini.

 Madenge akizungumza kabla ya semina kufunguliwa

 Dorothy akifungua semina hiyo.

 Baadhi ya wajumbe wakiwa ukumbini kwenye semina hiyo.

 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada kwenye semina hiyo.

 Mmoja wa wajumbe akiwahamasisha wenzake baada ya semina kufunguliwa.

Madenge akiagana na Dorothy baada ya semina kufunguliwa. (Picha na Bashiri Nkoromo)


HABARI KAMILI

 CCM MORO WAPONGEZA ZIARA ZA KINANA MIKOANI

*Mwenezi asema zianaimarisha, kujenga heshima ya chama

*Ataka Wana-CCM kuunga mkono ziara hizo 


BASHIR NKOROMO NA LATIFA GANZEL, MOROGORO
CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro kimepongeza ziara za katibu mkuu wa CCM Abduraharam  Kinana kwamba ziara hizo zimezidi kukiimarisha chama na kukiongezea heshima.

Katibu wa Itikadi na uenezi wa mkoa wa Morogoro Dorothy Mwamsiku alisema hayo wakati akifungu semina ya viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM,  wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, leo, katika ukumbi wa Road View Motel iliopo Nane nane manispaa ya Morogoro.


Aliwataka wanachama wa CCM nchi nzima kumuunga mkono Kinana na Sektetarieti yake kwa kusimamia na kutekeleza maagiizo aliyotoa katika ziara hizo ikiwemo kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM na kisikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kusitatua.

Katibu huyo alisema kuwa kuna kila sababu ya viongozi wa CCM kutokubali kuwafumbia macho watendaji wanaoshindwa kutekeleza ilani ya CCM kwa makusudi kwa lengo la kukikwamisha chama hiki.

Alisema   kuwa wapo watendaji ambao hawakitendei haki chama cha  Mapinduzi kwa, kufuja  fedha za miradi kwa makusudi .

'' Unakuta baadhi ya watendaji hawatekelezi ilani ya CCM ipasavyo na hivyo kusababisha CCM kusemwa vibaya, tusikubali, sisi tuwe wakwanza kuwashughulikia kabla ya sisi kunyoshewa vidole'' Alisema.


Hata hivyo alisema kuwa kuna kila sababu kwa viongozi wa CCM na wanachama kwa ujumla wanatambua miradi yote ya maendeleo iliopo ktika maeneo yao inavyoanza kutekelezwa ili ikitokea mtendaji anafanya ubadhilifu iwe rahisi kuwashughulikia.

Aidha alisema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali za baadhi ya watendaji wanaokwamisha utekelezaji huo wa ilani lakini  hadi sasa ilani hiyo imetekelezwa kwa kiasi kikubwa.
"Pamoja na utekelezaji huo bado wapo watu wanaosema CCM haijafanya kitu, kazi ya wapinzani kukosoa  na CCM kazi yatu kutenda, tusikate tamaa tusonge mbele.

Aliwataka jumuiya ya wazazi kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto kwa kuwa hiyo ndio moja ya malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo badala ya kuwaachia vijana wakiharibika na kutumbukia katika vitendo viovu vinavyopelekea kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Kwa upende wake Mwenyekiti wa CCM wilaya Kinondoni, Salumu Madenge ambaye ndiye Mwenyekiti wa semina hiyo, alisema,  lengo la semina hiyo ni kuwaweka viongozi hao katika mazingira ya ulelewa wa kutosha wa namna mbalimbali ya kutekeleza majukumu yao na wajibu wa kwa chama cha Mapinduzi.

Awali mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Kinondoni Charlse Mgonja alisema  katika semina hiyo mada mbalimbali zitatolewa ikiwemo umuhimu wa mchango wa jumuiya hiyo katika kuimarisha chama cha Mapinduzi, na historia na kusimamia maadili ya wanachama na viongozi ili kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya CCM na jumuiya zake. 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: CCM MORO WAFAGILIA ZIARA ZA KINANA MIKOANI, NI KATIKA SEMINA YA VIONGOZI WA WAZAZI KINONDONI.
CCM MORO WAFAGILIA ZIARA ZA KINANA MIKOANI, NI KATIKA SEMINA YA VIONGOZI WA WAZAZI KINONDONI.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmYmC7z-4xaWpV7J8iiOLhVp6BrKgtK_p533NJ6x7GEDzA2kHCI_OdQv4ubQ4r-MQSvl8C0i9jPYp2j4QFRVgDf5R8ye-fic15QS-l6zIm-aSgOp6tf6u9EfDPZHUG4urzoM-Pmjf21pw/s640/1.+Mgeni+rasmi+akiingia+ukumbini.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmYmC7z-4xaWpV7J8iiOLhVp6BrKgtK_p533NJ6x7GEDzA2kHCI_OdQv4ubQ4r-MQSvl8C0i9jPYp2j4QFRVgDf5R8ye-fic15QS-l6zIm-aSgOp6tf6u9EfDPZHUG4urzoM-Pmjf21pw/s72-c/1.+Mgeni+rasmi+akiingia+ukumbini.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2013/12/ccm-moro-wafagilia-ziara-za-kinana.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2013/12/ccm-moro-wafagilia-ziara-za-kinana.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy