WAZIRI MKUU PINDA AKATAA KUGOMBEA TENA UBUNGE

  (Juu na chini) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na mkewe Tunu (kushoto) wakisalimiana na watafiti wa masuala ya mazingira, wanawake na w...




 
(Juu na chini) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na mkewe Tunu (kushoto) wakisalimiana na watafiti wa masuala ya mazingira, wanawake na wanyamapori Profesa Tim Cars (wa pili kulia) na Profesa Monica Malder (wa pili kushoto) kijijini kwake Kibaoni wilayani Mlele Julai 19, 2015. Watafiti hao wenye makazi  yao kijijini hapo tangu 1995. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)






Na Mwandishi Wetu.

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa  jimbo lake la uchaguzi la Katavi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha.

Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele (Jumapili, Julai 19, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wengine nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.

Amesema yeye ataendelea kuwa karibu na wananchi wa Katavi wakati wote  na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

Mheshimiwa Pinda aliwaasa wananchi wa jimbo la Katavi wawe makini katika kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao.

Akimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, Paroko wa Parokia ya Usevya wilayani Mlele, Padri Aloyce Nchimbi aliwaasa wananchi wa Wilaya ya Mlele kumuenzi Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hata atakapokuwa amestaafu kwani bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea maendeleo.

Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Jana saa 10 jioni ndiyo ilikuwa mwisho wa kurejesha fomu za ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU PINDA AKATAA KUGOMBEA TENA UBUNGE
WAZIRI MKUU PINDA AKATAA KUGOMBEA TENA UBUNGE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHMioHml3goF1EvQbQzN40TdnTOE4Bq8u3sCFqy1VKhKngBJMjxi48pG4GWk3DzXiIbnrH8oljx9iybH4bNBXxyI42QCcKq285vTTTSrPLIi0rWh4mzKR4T9pvLEiPjErykB8kGusYK_5c/s640/IMGL6627.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHMioHml3goF1EvQbQzN40TdnTOE4Bq8u3sCFqy1VKhKngBJMjxi48pG4GWk3DzXiIbnrH8oljx9iybH4bNBXxyI42QCcKq285vTTTSrPLIi0rWh4mzKR4T9pvLEiPjErykB8kGusYK_5c/s72-c/IMGL6627.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2015/07/waziri-mkuu-pinda-akataa-kugombea-tena.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/07/waziri-mkuu-pinda-akataa-kugombea-tena.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy