Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwa Rais n...
Rais
Jakaya Kikwete akimwapisha Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi
Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
|
Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi
akitia sahihi baada ya kuapa.
|
Rais
Jakaya Kikwete akitia sahihi kiapo hicho.
|
Rais
Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi.
|
Rais
Jakaya Kikwete akimpongeza kwa baada ya kupokea vitendea kazi hivyo.
|
Rais Jakaya Kikwete
akiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu Jaji Francis Mutungi (kushoto)na Msajili wa
Vyama vya Siasa Mstaafu, John Tendwa (kulia) baada ya kumuapisha Jaji Mutungi Ikulu.
|
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa
Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu
Dar es Salaam leo. (PICHA NA IKULU)
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya
leo, Jumatatu, Agosti 26, 2013, amemwapisha Jaji Francis Sales Katabazi Mutungi
kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa mpya.
Jaji
Mutungi anachukua nafasi ya John Tendwa ambaye amestaafu kutoka Utumishi wa
Umma kwa mujibu wa sheria.
Sherehe
za kumwapisha Jaji Mutungi zilizofanyika Ikulu, Dar Es Salaam zimehudhuriwa pia
na Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi, Fakhi Abdallah Rheno Jundu
pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
COMMENTS