KATIBU MKUU UVUVI ATEKETEZA NYAVU HARAMU ZA BILIONI 2.6 MWANZA

Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na ki...



Shehena
ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa
katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu
kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa
jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,. (Picha na John
Mapepele)
Shehena
ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa
katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu
kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa
jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John
Mapepele


Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akishiriki kwenye zoezi la kuteketeza
nyavu haramu za uvuvi  zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6
zilizokamatwa
katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu
kilichoundwa
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu
kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa
jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto kulia mwenye suti ni
Katibu
Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia
Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana
Budeba
akishuhudia,Picha na John Mapepele


Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana
Budeba wa kwanza kulia aliyevaa suti akishirikiana na Mkuu wa wilaya
ya Nyamagana,Mary Tesha
zoezi la kuteketeza nyavu haramu za
uvuvi  zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa
katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu
kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa
jina la operesheni Sangara
,Picha na John Mapepele
Na
John Mapepele, Mwanza.


Katibu
Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana
Budeba ametaifisha na kuteketeza zaidi ya tani mia mbili za shehena
ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa
katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu
kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa
jina la operesheni Sangara .

Mbali
na kuteketeza zana hizo haramu, Serikali pia imekusanya zaidi ya shilingi
bilioni tano kama sehemu ya adhabu  kwa wavuvi na wafanyabiashara
waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji mwani, samaki
na mazao yake nje ya nchi.

Akizungumza
na mamia ya wavuvi wakati wa kuteketeza nyavu hizo leo, katika dampo
la Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza, Dkt. Budeba amesema hatua
hizo kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi
kuwaonea wafanyabiashara au wavuvi wanyonge bali zimelenga kuwatengenezea
maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali
zilizoko ziwani.

Aidha
Dkt. Budeba amesisitiza kuwa kikosi hicho kitaendelea na operesheni
hiyo bila kuchoka hadi hapo uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi
utakapokwisha ndani ya ziwa hilo.

Pia
aliwaonya wamiliki wa  viwanda na wafanyabiashara wanaotengeneza
na kuuza nyavu hizo ambapo amesema Serikali ikiwabaini itawachukulia
hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na  kuwafutia leseni zote
za biashara zao.


Alisema rasilimali  zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi
viongozi wamepewa dhamana ya kuongoza kazi ya ulinzi tu na endapo uvuvi
haramu utakomeshwa wananchi ndiyo watakaonufaika.

Pamoja
na kuteketeza nyavu hizo haramu, Dkt Budeba alieleza hali ya upatikanaji

wa samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu

wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)
mwaka 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia
96.6  hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo
samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi
na hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio
wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi, Fatma Sobo amesema Idara itaendelea kutumia Sheria ya Uvuvi
namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na Sheria
nyingine za Mazingira ili kudhibiti Uvuvi haramu nchini.

Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha alisema Serikali ya Wilaya
hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na
kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi
haramu ili kulinda rasimali  hiyo muhimu waliyopewa na
Mungu.

Kwa upande wao baadhi ya
wavuvi walimuomba Dkt. Budeba kuwasiliana na Wizara ya Viwanda na Biashara,
ili kuona namna ya kudhibiti nyavu zisizoruhusiwa ambazo zinatengenezwa
viwandani na baadae kuuziwa wavuvi.

Hivi karibuni watendaji
wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana  na kikosi
kazi kilichoundwa na Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi  wameweza
kukamata  nyavu haramu, meli za uvuvi kutoka nje ya nchi zinazovua
bia kufuata taratibu na mazao ya uvuvi yanayotoroshwa nje ya nchi ikiwemo
mwani na samaki yenye mabilioni ya fedha huku Waziri Mwenye dhamana
ya sekta hiyo Luhaga Mpina kuahidi kuwa  operesheni hizo zitakuwa
za kudumu hadi uuvi haramu utakapokoma.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KATIBU MKUU UVUVI ATEKETEZA NYAVU HARAMU ZA BILIONI 2.6 MWANZA
KATIBU MKUU UVUVI ATEKETEZA NYAVU HARAMU ZA BILIONI 2.6 MWANZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4K32ISZV4lC7jmVvdjLzhNNuNDypTacAV4bHGLAeJ4liB4QbPAb6S0LEJWyDjMI9zaw4zgFFiYaPu5iLSPgdrpHnnKYaWxaBXPOyMt2vauX7Vys6oBr8R0nwpLB32_F8j6ghcx0w35uFb/s640/IMG-20180204-WA0002.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4K32ISZV4lC7jmVvdjLzhNNuNDypTacAV4bHGLAeJ4liB4QbPAb6S0LEJWyDjMI9zaw4zgFFiYaPu5iLSPgdrpHnnKYaWxaBXPOyMt2vauX7Vys6oBr8R0nwpLB32_F8j6ghcx0w35uFb/s72-c/IMG-20180204-WA0002.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/katibu-mkuu-uvuvi-ateketeza-nyavu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/katibu-mkuu-uvuvi-ateketeza-nyavu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy