Kaimu Afisa Mtendaji wa Kampuni ya Simu Tanzania, (TTCL), Peter Ngota, (kulia), akimkabidhi cheti Kaimu Mkurug...
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kampuni ya Simu Tanzania,
(TTCL), Peter Ngota, (kulia), akimkabidhi cheti Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD,
Cosmas Mwaifani wakati wa hafla ya kukabidhi mradi wa mkongo wa simu kwa idara
hiyo ya hifadhi ya madawa nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo
Ijumaa Julai 24, 2015. TTCL imekamilisha mradi wa kuiunganisha idara ya taifa
ya hifadhi ya madawa, (MSD), na mkongo wa mawasiliano (fibre-optic) na sasa
makao makuu ya MSD yanaweza kuwasiliana kwa haraka kupitia teknolojia hiyo mpya
yenye kasi ya ajabu.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Simu Tanzania, (TTCL), Peter Ngota, akionyesha mashirika na nchi ambazo
tayari zimeunganishwa na mkongo huo wa taifa wa mawasiliano
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifani, akitoa hotuba ya kuupokea mradi huo
Picha ya pamoja ya watumishi wa TTCL na wenzao wa MSD. (Imeandaliwa na K-VIS Blogs)
COMMENTS