Meya Jerry Slaa akifuatilia kwa karibu burudani zilizokuwa zinatolewa na vikundi mbalimbali katika mkutano huo. Pmaoja naye ni Mjum...
![]() |
Meya Jerry Slaa akifuatilia kwa karibu burudani zilizokuwa zinatolewa na vikundi mbalimbali katika mkutano huo. Pmaoja naye ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Mh Adam Kimbisa |
NA MWANDISHI WETU
-Atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la
Ukonga
Diwani wa kata ya Gongo
la Mboto,Jerry Slaa ameainisha mafanikio aliyotekeleza katika kipindi cha miaka
5 tangia achaguliwe kuwa Diwani na Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo pia
alitimiza ahadi mbalimbali alizokuwa ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya
Ilala.
Slaa alivipatia msaada
wa fedha vikundi vya VICOBA alivyokuwa ameviahidi kuvisaidia,Genereta za kutoa
nishati za kuendeshea miradi kwa vikundi kwenye maeneo yasio na umeme,vifaa ya
michezo kwa vijana na hati za uthibitisho wa ujenzi wa barabara
zitakazojengwa kwa madiwani wa kata za jimbo la Ukonga.
Slaa ambaye pia ni
mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi alitangaza mafanikio hayo katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi ya Kitunda iliyopo jimbo
la Ukonga jana ambapo pia alitangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo la
Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba
mwaka huu.
Baadhi ya
mafanikio aliyofanikisha katika kipindi cha uongozi wake aliyabainisha kuwa ni
katika sekta ya elimu- ambapo mazingira katika shule mbalimbali yameboreshwa,afya-ambapo
vituo vipya vimejengwa na vingine
kupatiwa vifaa na dawa,miradi ya maji na
ujezi wa barabara kwenye kata ya Gongo la Mboto na kata zote za Manispaa
ya Ilala.
“Kutokana na mafanikio yaliyopatikana nawaomba wananchi wa jimbo la
Ukonga mniunge mkono kwa kinichagua niwe Mbunge wenu katika uchaguzi mkuu ujao
ili nizidi kuwatumikia na kushirikiana nanyi kuleta maendeleo katika jimbo hili
la Ukonga ambalo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali za maendeleo”Alisema.
Alisema wakazi za jimbo la Ukonga wanahitaji
Mbunge ambaye atakuwa bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea
maendeleo wananchi. “Bado tunahitaji kuboresha zaidi huduma za kijamii
kama vile shule, hospitali ,maji safi,kubuni miradi ya maendeleo ya
akina mama na vijana kwa kuwa naelewa matatizo ya jimbo hili na baadhi
yake nilishaanza kuyavalia njuga nikiwa diwani, mkinichagua kuwa mbunge wenu
nitaendeleza safari ya kuleta maendeleo.”
Mkutano huo wa Meya Jerry Slaa ulihudhuriwa na mamia ya wakazi
wengi wa jimbo la Ukonga ambao wengi wao walipokea tamko hilo la kutangaza nia
kwa furaha na baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa kiongozi huyo anaelewa
matatizo ya wananchi wa Ukonga na ni mtu wa watu ambaye amekuwa akitekeleza
majukumu yake ya kazi kwa kujali watu wa aina zote.
2.Mmoja wa wawakilishi wa
kikundi cha akina mama akipokea fedha kwa niaba ya wenzake kutoka kwa Meya wa Manispaa ya ilala ambazo alikuwa amewaahidi wakati wa mkutano
wa Meya huyo kuelezea mafanikio yake.
3.Baadhi ya madiwani na
wazee wa Ukonga wakimpongeza Meya Jerry Slaa kwa kutimiza ahadi alizotoa muda mfupi
baada ya kueleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake ambapo vilevile
alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga
4.Watoto wakitoa burudani
wakati wa mkutano huo
5.Baadhi ya madiwani na
viongozi wa CCM kata ya Ukonga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano
huo
6.Sehemu ya umati wa watu
waliohudhuria mkutano huo wakishangilia kwa furaha baada ya kuguswa na hotuba
ya Meya Jerry Slaa
7. .
COMMENTS