Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga baada ya kumkabidhi taarifa ya ...
*****************
WAZIRI
MKUU AWAPA POLE WAFIWA, AWAFARIJI MAJERUHI KAHAMA
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametembelea baadhi ya familia zilizopoteza wapendwa wao pamoja na majeruhi waliolazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana na maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia jana.
Akizungumza na wafiwa katika vijiji vya Mwakata na Magugung’hwa katika kata ya Mwakata wilayani Kahama leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015) Waziri Mkuu alisema Serikali haitawaacha katika kipindi hiki kigumu walichonacho.
Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuwafikishia wafiwa na waathirika
wa maaafa hayo salamu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye aliwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Akiwa katika shule ya msingi Mwakata ambako watu 250 wanahifadhiwa hapo kwa muda, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao pamoja na wananchi waliofika kumsikiliza kwamba Serikali imepanga kuleta vyakula, mahema, mablanketi na madawa ya hospitali ili kuwasaidia waathirika hao.“Serikali haitaacha mtu afe kwa njaa,” alisema.
Pia aliagiza maghala ya NFRA yaliyoko Isaka yatumike kupokea misaada ya chakula kwa sababu yako karibu sana kata ya Mwakata. “Ili uratibu wa misaada uweze kufanyika hapa kijijini, ni vema maghala ya kuhifadhi chakula cha msaada yakahamia hapa Isaka kwa sababu ni karibu sana na hapa Mwakata,” alisema.
“Yakiwa hapa itasaidia usimamizi na uhakika wa huduma zinazotolewa kwa waathirika. Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya simamieni hilo kwa sababu janga hili ni letu na linabebwa na Serikali,” aliongeza.
Alisema ameongea na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid na kumwagiza atume watu wake wafanye tathmini ya hali ya afya kwani katika hali ya majanaga kama haya, ni lazima kuna hatari ya kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.
Mapema, Mbunge wa Msalala, Bw. Ezekiel Maige aliiomba Serikali itume misaada ya haraka ya vyakula na mahema kwa waathirika hao lakini pia ipeleke kikosi cha wanajeshi ili wasaidie kujenga nyumba za watu walioathirka kama ambavyo ilifanya kwa watu wa Kilosa mwaka 2009.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge), Bibi Jenista Mhagama ambaye anasimamia idara ya
maafa ameuagiza uongozi wa wilaya ya Kahama kuhamishia timu ya
waratibu wake kwenye eneo la tukio badala ya kufanyia kazi kutoka
makao makuu ya wilaya ambako ni zaidi ya km. 30.
“Misaada iasche kuratibiwa wilayani bali ihamie hapa Mwakata, na hao wanaotoa misaada waambiwe wailete hapa kwenye eneo la tukio … uratibu ukifanyika kule hakuna atakayekuwa na picha halisi ya nini kinaendelea kwenye kijiji hiki,” alisisitiza.
Mvua hiyo imesababisha vifo vya watu 42 na kujeruhi watu 98 huku mamia watu wakiwa hawana mahali pa kuishi. Pia watu 52 kati ya 112 waliokuwa wamelazwa hospitalini wameruhusiwa kurudi majumbani huku majeruhi 60 wakiendelea kupatiwa matibabu.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MACHI 5, 2015.

**********************
WAZIRI MKUU AZINDUA TAARIFA YA BRN
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuwa Serikali itahakikisha kuwa sekta na miradi inayotambuliwa na kuingizwa kwenye Mfumo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now au BRN) ni ile yenye manufaa makubwa nay a haraka kwa wananchi walio wengi.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015) wakati
akizungumza wa wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya mwaka wa kwanza ya utekelezaji wa Mfumo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa kwenye uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar es Salaam.
“Vigezo hivi ndivyo vilivyotumika kutambua sekta sita za mwanzo ambazo ni kilimo, elimu, nishati, uchukuzi, utafutaji rasilmali fedha na maji ambazo leo ndiyo tunapokea taarifa ya utekelezaji wake kwa mwaka wa kwanza,” alisema.
Alisema vigezo hivyo pia vilitumika kuchagua mazingira ya biasharana
huduma za afya kuziingiza kwenye utaratibu wa BRN. “Serikali inaamini
kwamba kuimarika kwa mazingira ya biashara, hasa biashara ndogondogo, kutatoa fursa za watu wengi zaidi kujiajiri na kuajiri na kuajiri wengine,” aliongeza.
Alitoa wito kwa watendaji wote kujifunza na kuutumia mfumo huo ili
waweze kufikia malengo waliyojiwejkea kwa haraka zaid. “Mambo matatu
yanayoupa mfumo huu uwezo mkubwa zaidi ni kupanga kipaumbele; kuwa na nidhamu na uwazi; na haya mambo yako ndani ya uwezo wa kila Mmoja wetu,” alisema.

Alisema Serkali itaendelea kuchukulia
utekelezaji wa mfumo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa kama jambo la
kipaumbele katika kutekeleza majukumu yake.
“Haitoshi kwamba tumepata mafanikio haya katika mwaka Mmoja. Ni lazima sasa tuazimie sote kuchukua kanuni hizi na kuzitumia katika kila eneo la maisha yetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tumetoa mchango kamili kwa Taifa letu kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ta Maendeleo hadi mwaka 2015,” alisema.
Alitumia fursa hiyo kuwashukuru Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa
halmashauri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri kwa kusimamia vema utekelezaji wa BRN katika maeneo yao.

Mapema, akimkaribisha Waziri
Mkuukuzungumza na washiriki kabla ya
kuzindua taarifa hiyo, Mtendaji Mkuu wa Presidential Delivery Bureau,
Prof. Issa Omari alisema utoaji wa taarifa hiyo ni hatua mojawapo kati
ya hatua nane za mfumo huo. Aliwataka watendaji wanaotekeleza mfumo huo wahakikishe wanafuata hatua zote nane.
Alisema kwamba jambo msingi katika utekelezaji wa BRN ni kubadilisha
maisha ya wananchi na siyo tu kupima utendaji kazi wa mawaziri wa
sekta husika.
Alisema mojawapo ya mafanikio ya utekelezaji wa mfumo huo ndani ya
mwaka mmoja ni ushirikishwaji wa jamii kwa kiwango kikubwa kiasi cha kusaidia kasoro za kijamii. “Kwa mfano katika sekta ya elimu, watu
wanashangaa ufaulu kupanda haraka… lakini tuna shuhuda za utoro
kupungua kwenye shule moja kutpoka watoto 500 hadi sifuri…. Hii ni kwa sababu tuliishirikisha jamii hadi ngazi ya chini,” alisema.
Waziri Mkuu ameenda Kahama, mkoani Shinyanga kuwapa pole waathirika wa maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia jana. Mvua hiyo imesababisha vifo vya watu 92 na kujeruhi watu 98 huku mamia watu wakiwa hawana mahali pa kuishi.

COMMENTS