USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA OPERESHENI YA ULINZI WA AMANI DRC Mkurugenz...
USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA OPERESHENI YA ULINZI WA AMANI DRC
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari
wakimsikiliza wakichukua taarifa za wasemaji hao. (Picha
na Anna Nkinda – Maelezo)
|
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Erick Komba akiongea na waandishi wa habari leo kuhusu ushiriki huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah Mwambene. |
Ushiriki wa Tanzania katika
Operesheni ya Ulinzi wa Amani nchini DRC, unatokana na mgogoro kati ya Serikali
DRC na waasi hususan kikundi cha waasi cha M23. Mgogoro huo ulianza mwezi Aprili
2012 ambapo kikundi cha M23 kilijitoa katika Jeshji la serikali ya DRC na
kuanzisha mapigano hali iliyopelekea hali ya usalama nchini DRC kuwa mbaya.
Kufuatia hali hiyo mbaya ya usalama,
wakati wa kikao cha International Conference on the Great Lakes Region
kilichofanyika tarehe 12 Julai 2012 mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mhe. Rais
Joseph Kabila aliwasilisha ombi kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu ambazo
Rwanda, Uganda, Tanzania, na DRC akaomba
nchi wanachama wa Maziwa Makuu zisaidie kuwapokonya silaha waasi wa M23.
Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu
walikubaliana na ombi hilo na kutoa maelekezo kwa Mawaziri wa Ulinzi ambao
walikutana tarehe 01 hadi 2 Agosti 2012
na kujadili maelekezo ya Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu. Mawaziri wa
Ulinzi walikubaliana kuwa ni muhimu kwa vikundi vyote vya Waasi (ADF, FDLR na
M23) kushughulikiwa na wakawasilisha mapendekezo yao kwa Wakuu wa Nchi za
Maziwa Makuu.
Tarehe 7 Agosti 2012, Wakuu wa nchi
za Maziwa Makuu walikutana tena mjini Kampala, Uganda na kupanga mkakati wa
kuanzishwa kwa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ na nchi wanachama wa Nchi za
Maziwa Makuu zikaombwa kuchangia askari watakaounda ‘Neutral Intervention Force
(NIF)’ ambapo Tanzania iliombwa na ikahadi kuchangia kikosi kimoja. Kikao hiki
kilitoa maelekezo ya hatua inayofuata kwa Mawaziri wa Ulinzi wa Maziwa Makuu.
Tarehe 7 hadi 8 Sep 2012, Mawaziri wa
Ulinzi wa maziwa Makuu, walikutana na kujadili utekelezaji wa uanzishwaji wa ‘Neutral
Intervention Force (NIF)’. Wakaunda ‘Military Assessment Team (MAT)’ kufanya
tathmini ya tishio. Timu hiyo ililifanya tathmini na kuwasilisha taarifa yake
kwenye kikao cha Mawaziri wa Ulinzi kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2012 mjini
Goma, DRC na baadaye taarifa hiyo iliwasilishwa kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa
Makuu ambao waliagiza kushirikishwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya maendeleo
kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika(AU) na Umja wa Mataifa(UN) ili kufanikisha
mkakati huo.
Nchi wanachamma wa SADC na Nchi za
Maziwa Mkuu kwa pamoja walikubaliana na kupendekeza SADC Standby Brigade
ipelekwe DRC kama ‘Neutral Intervention Force (NIF)’. Kufuatia ridhaa hiyo nchi
wanachama wa SADC ziliombwa kuchangia ambapo nchi mbalimbali wanachama
zilikubali kuchangia, lakini Umoja wa Mataifa(UN) ilizipitisha nchi za
Tanzania, Afrika Kusini na Malawi kuchangia askari nguvu ya Brigedi moja kuunda
NIF ya MONUSCO.
Aidha, Umoja wa Mataifa mwezi Januari
2013 uliridhia mapendekezo ya Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu na Nchi wanachama
wa SADC ya kuundwa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ na kupelekwa DRC. Kufuatia
idhini hiyo tarehe 28 Machi 2013, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
lilipitisha Azimio (Resolution)
namba 2098 (2013) na kutoa jukumu maalumu la ulinzi wa amani nchini DRC,
likijumuisha ushiriki wa Neutral Intervention Force (NIF) kama sehemu ya
MONUSCO, na ikaitwa ‘Force Intervention Brigade (FIB)’ ambayo kikosi cha
Tanzania ni sehemu ya Brigade hiyo.
Kwa mantiki hiyo ieleweke kwamba,
Kikosi cha Tanzania kilichopo DRC ni sehemu ya SADC standby brigade iliyotoa
mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO). Kinafanya kazi chini
ya Force Commander, MONUSCO na majukumu yake ni:
a. Kuzuia waasi kujitanua (Prevention of Expansion)
b. Kuvunja nguvu za waasi (Neutralization)
c. Kuwapokonya silaha makundi yote ya waasi.
Kwa kuzingatia kuwa kikosi chetu kiko
chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa ya MONUSCO, inamanisha kuwa Operesheni
hiyo ni ya Umoja wa Mataifa, Tanzania
haipigani na M-23 na haina tatizo na Rwanda kuhusiana na Operesheni hiyo na
ridhaa ya kikosi chetu kwenda DRC ilikubaliwa pia na Rwanda, nchi ambayo ni
mwanachama wa nchi za Maziwa Makuu. Aidha, Rwanda imesaidia sana kwa kuruhusu
kikosi cha Tanzania kupitisha watu, vifaa na zana katika nchi yake kupeleka
DRC.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.
COMMENTS