AJALI YA MOTO KWENYE MITAMBO YA SONGAS KUWAACHA BAADHI YA WAKAZI WA DAR GIZANI KWA WIKI NZIMA

  Askari wa Kikosi cha zimamoto wa knight support na halmashauri ya jiji la Dar es salaam wakizima moto huo Dar es Salaam jana. ...



 
Askari wa Kikosi cha zimamoto wa knight support na halmashauri ya jiji la Dar es salaam wakizima moto huo Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu
MOTO mkubwa uliozuka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas Ubungo, Dar es Salaam, umeathiri mitambo na vifaa vya umeme na kusababisha baadhi ya maeneo ya Jiji hilo, kukosa umeme, hali inayotarajiwa
kuchukua zaidi ya wiki moja.

Maeneo hayo kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba, yatahusu wilaya za Ilala na Kinondoni.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo maeneo yatakayoathirika ni Mwenge, Magomeni, Tandale, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Changanyikeni, Kimara, M

bezi, Tabata, na Ubungo River Side.
Mkurugenzi huyo aliwafafanulia wanahabari kwamba ajali hiyo ya moto ulizuka saa 9.45 alfajiri na
kuunguza nyaya za kusafirishia umeme kutoka mitambo hiyo, hali iliyosababisha Jiji la Dar es Salaam kukosa umeme kuanzia saa 10 alfajiri.
Mramba alisema kwamba moto huo ambao hadi sasa chanzo chake hakijafahamika, askari wa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji kwa kushirikiana na kikosi cha wazimamoto na waokoaji binafsi
wa Night Support, walifanikiwa kuuzima kabla haujasambaa kwenye mitambo mingine.
“Hadi sasa hatujabaini chanzo cha moto huu na uchunguzi unaendelea, tunachoweza kusema
sasa ni tunachokiona kwa macho, kwamba kuna nyaya zimeungua… baada ya uchunguzi kukamilika
tutatoa taarifa,” Alisisitiza Mkurugenzi.


Pamoja na kuungua kwa nyaya hizo, alisema baadhi ya
vifaa kwenye vituo vidogo vya umeme pia vimeungua na shirika litatoa taarifa kamili ya mali zilizoharibiwa
na moto huo, uchunguzi ukikamilika.

Alisema shirika kwa sasa linajitahidi kuhakikisha hali katika eneo hilo, inarejea kawaida kwa kuanza
na uhakiki wa ukubwa wa tatizo na kuangalia vifaa vilivyoharibika ambavyo vinahitaji kurudishwa
upya ikiwamo nyaya kutandazwa upya.

Aliwaomba radhi wateja na wanachi wote kwa usumbufu utakaokuwa umejitokeza kwa tukio hilo na kuwataka watoe ushirikiano kwa Tanesco ili umeme uweze
kurudi haraka.

Mramba aliongeza kwamba uhakiki wa haraka
kazi hiyo inatarajiwa kukamilika baada ya wiki kadhaa.
“Hii si kazi ya saa kadhaa au siku moja, mafundi watakapoanza kazi tutajua vitu vilivyoungua na
vinakopatikana na tutakachokifanya ni kuangalia namna ya kuwapa watu umeme kutoka vituo vingine,” alisema.
Pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, aliyetembelea mitambo hiyo baada ya kupata taarifa za moto, aliagiza shirika hilo kuhakikisha uchunguzi wa haraka unafanyika na kutoa taarifa
kuhusu sababu za moto huo.
“Lakini pia katika maeneoambayo yataathiriwa kwa kukosa umeme, jitihada zifanyike iliwarejeshewe waendelee na shughuli zao za kawaida,” alisisitiza.
Taarifa kuchelewa kwa upande wa Kamanda wa
Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jesuald Ikonko, alisema kikosi chake kilipokea taarifa za kuungua mitambo hiyo saa 11.58 alfajiri na
walifika eneo la tukio saa 12.05
asubuhi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AJALI YA MOTO KWENYE MITAMBO YA SONGAS KUWAACHA BAADHI YA WAKAZI WA DAR GIZANI KWA WIKI NZIMA
AJALI YA MOTO KWENYE MITAMBO YA SONGAS KUWAACHA BAADHI YA WAKAZI WA DAR GIZANI KWA WIKI NZIMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0U2EYGyC1UJWiNHBUFdvqF2R_inMnOCR39ezvd6oD5ycC9F_05-yTLvwzCQr2D6AHEZeZ_6PV8Av3rdgNAmQiSHyD5YUmryF3TIyMdFMN1dAHbwrmD_nYv9Fk9NREpkw1KDWjvk7L7M-0/s1600/IMG_2548.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0U2EYGyC1UJWiNHBUFdvqF2R_inMnOCR39ezvd6oD5ycC9F_05-yTLvwzCQr2D6AHEZeZ_6PV8Av3rdgNAmQiSHyD5YUmryF3TIyMdFMN1dAHbwrmD_nYv9Fk9NREpkw1KDWjvk7L7M-0/s72-c/IMG_2548.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2013/08/ajali-ya-moto-kwenye-mitambo-ya-songas.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2013/08/ajali-ya-moto-kwenye-mitambo-ya-songas.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy