Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akizungumza na washiriki wa kambi ya vijana Julai 30 Dar es Salaam al...
Baadhi ya washiriki wa kambi ya vijana wakisikiliza Waziri Fenella Mukangara alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo. |
Baadhi ya washiriki wa kambi ya vijana wakisikiliza Waziri Fenella Mukangara alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo.
|
Kikundi cha sanaa kutoka IYF wakicheza muziki wa kitamaduni kutoka Korea mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara wakati wa hafla hiyo.
|
Kikundi cha sanaa kutoka IYF wakicheza muziki wa kitamaduni kutoka Korea mbele ya Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara wakati wa hafla ya ufunguzi kambi hiyo.
|
Waimbaji wa Kwaya ya kimataifa kutoka Korea Gracias wakiimba wakati wa hafla ya ufunguzi.
|
Kikundi cha sanaa kutoka Tanzania wakionyesha mchezo wa Tai Kondo.
|
Na Frank Shija - Maelezo
Vijana nchini wameaswa kujitambua na kuthubutu kwa malengo chanya pamoja ikiwa ni pamoja na kujituma kufanya kazi zikiwemo za kujitolea kwa kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kujikwamua na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla..
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara alipokuwa akifungua kambi ya dunia ya vijana leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Fenella amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakiishi kwa mazoe na kufuata mikomba ambapo ni hatari sana matokeo yake wamekuwa wakijikuta wakitenda tofauti na malengo yao.
Aliongeza kuwa ni wakati sasa kwa vijana kujitambua na kubadilisha fikra zao hili waweze kujiletea maendeleo wao wenyewe baadala ya kulalamika kama ambavyo wamekuwa wakifanya.
"Ni muhimu vijina mjitambue na mthubutu kwa malengo chanya, na muanze kwa kila mmoja wenu kujituma kufanya kazi na wakati mwingine jitoleeni kwa faida ya jamii zenu". Alisema Waziri Fenella
Aliongeza kuwa Mungu amewajali vijana Talanta na vipaji tofauti hivyo ni muhimu vikatumika kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla na kuongeza kuwa kujitambua kwa vijana kuendane na uthubutu ili kujikwamu kimaendeleo.
Kwa upande wake mwanzilishi wa IYF duniani Pastor Park Ock Soo amesema kuwa ni faraja kwake kuona vijana wengi wamejitokeza kushiriki kambi hiyo akiamini malengo ya kuanzishwa kwa taasisi yake yamefikiwa kwa kiasi kikubwa.
Pastor Park ameongeza kuwa vijana wanapaswa kubadili fikra na mitazamo yao ili kuenenda na kasi ya kujiletea maendeleo badala ya kulalamika na kusubiri kufanyiwa kazi.
Kambi hii ya vijana ni inafanyika hapa nchini kwa mara ya tano na imeandaliwa na taasisi ya International Youth Fellowship (IYF) kutoka Korea kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni "Badilisha Fikra ktuoka mtazomo hasi kuw chanya"
COMMENTS