Mtafiti wa Masoko ya Ajira, VETA Makao Makuu Julius Paul Mjelwa akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye Maonyesho ...
|
Mtafiti wa Masoko ya Ajira, VETA Makao Makuu Julius Paul Mjelwa akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), kuhusu huduma na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na vyuo vya VETA.
|
|
Mhandisi Adrian Kashula wa VETA Kipawa Dar es Salaam, akitoa maelezo kuhusu teknolojia ya kisasa ya umeme wa viwandani ambayo inatumia eneo dogo na kutoa taarifa pale panapotokea hitilafu, akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda hilo.
|
|
Mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa VETA Chang'ombe Dar es Salaam, fani ya uchoraji ramani na usanifu majengo, Fatma Mohamedi akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya taaluma hiyo yanayotolewa na chuo hicho katika ngazi mbalimbali.
|
|
Baadhi ya mashine na mitambo inayozalishwa na vyuo mbalimbali vya VETA nchini, ambayo ikitumika vema inaweza kulikomboa taifa kiuchumi kwa kuepuka utegemezi wa mashine na mitambo kutoka nje.
|
|
Mkufunzi wa Ufundi wa VETA, Sirili Aloyce akionyesha mojawapo ya mashine zinavyofanya kazi. Kwa mujibu wa tekinolojia hiyo, Sauti hutumika kuzalisha umeme pia. Huo ni miongoni mwa ugunduzi na utafiti uliofanywa na VETA.
|
|
VETA imebuni teknolojia ya kuzalisha umeme kwa kutumia betri, hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya dizeli na petrol kwa jenereta. Mwanafunzi wa VETA wa Mitambo na Mashine, Emmanuel Ngowo akionyesha jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
|
|
VETA wamekuja na jibu kupitia Chuo chao cha Dakawa, Morogoro kinachotoa mafunzo ya usindikaji na uzalishaji wa bidhaa za ngozi vikiwemo viatu vya aina mbalimbali. Mwanafunzi wa VETA, Onesmo Mrisho akitoa maelezo jinsi wanavyozalisha bidhaa za ngozi.
|
|
Mwanafunzi wa VETA, Theopista Michael akitoa maelezo wa wageni waliotembelea banda la VETA kuhusu mafunzo ya hoteli na utalii yanayotolewa na vyuo vya VETA vya Dodoma na Njiro mkoani Arusha.
|
|
Unajua mvinyo unatakiwa kuendana na aina ya chakula. Huyo ni Mwalimu Theonestina Raphael wa VETA Njiro, Arusha akielezea mvinyo Mwekundu na vyakula unaoendana navyo.
|
COMMENTS