Rais Jakaya Kikwete akizindua kitabu cha kampeni ya lishe Tanzania baada ya kukizindua Mei 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja Da...
|
Rais Jakaya Kikwete
akizindua kitabu cha kampeni ya lishe Tanzania baada ya kukizindua
Mei 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja Dar es
Salaam. Kulia ni Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo akifuatiwa na Mkurugenzi wa kwanza
wa Taasisi ya Chakula na lishe Mzee Lema. Kushoto ni
Mama Salma Kikwete na Mama Maria Nyerere.
|
|
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Rais
Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo maalum iliyotolewa na Taasisi ya Chakula
na Lishe kutambua mchango wake mkubwa katika kusimamia lishe na maendeleo yake
nchini. Kushoto ni Mama
Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere.
|
|
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid
akisalimiana kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania baada ya kukizindua. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mama
Salma Kikwete (kushoto) akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
|
|
Mama Maria Nyerere akifurahia tuzo maalumu
aliyopokea kwa niaba ya Baba wa Taifa aliyotunukiwa na Taasisi ya Chakula na
Lishe kwa mchango wake mkubwa kwa kukuza na kuendeleza sera ya lishe nchini
wakati wa sherehe za uzinduzi huo.
|
|
Rais Dk Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kwa komputa mpakato kuzindua filamu ya udumavu wakati wa uzinduzi wa lishe bora katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam. Kushoto kwake ni mke wake Mama Salma Kikwete, Waziri Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
|
COMMENTS