Wasanii wa kundi la Mrisho Mpoto wakiburudisha kwa ngoma za asili wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikoche...
|
Wasanii wa kundi la Mrisho Mpoto wakiburudisha
kwa ngoma za asili wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki
Mikocheni, Dar es Salaam, leo Machi 16, 2013
|
|
BURUDANI TENA HIYO |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kati),
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk Seif Rashid (wa pili kushoto), Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hurber
Kairuki, Dk Salim Ahmed Salim (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Shirika la Afya na
Elimu la Mikocheni Kokushubira Kairuki (kushoto kwa Rais) na Mkurugenzi Mkuu wa
hospitali hiyo Dk. Asser Mchomvu.
|
|
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la
kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malalusa (aliyepunga mkono) na viongozi mbalimbali
wa dini wakiwa katika sherehe hiyo.
|
|
Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Elinaza Sendoro akiswali kabla ya kuanza kwa sherehe. |
|
Sheikhe wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad
Musa Salum naye aliyemwakilisha Mufti wa Tanzania, Shaaban Bin Simba akiomba
dua kabla ya sherehe pia.
|
|
Wasanii wa kundi la Mrisho Mpoto wakiwa na picha ya Mwasisi wa hospitali hiyo, Hayati Profesa Hubert Kairukii |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akibonyesha kitufe cha kompyuta kuzindua mfumo wa TEKNOHAMA wa kuhudumia na
kutunza kumbukumbu za wagonjwa
|
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimkabidhi tuzo Dk Karungi Karoma aliyezaliwa kwenye hospitali hiyo
ilipoanzanzishwa ambapo wengine takribani ishirini hivi walikabidhiwa tuzo
katika sherehe hiyo.
|
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati
aliyeketi), viongozi mbalimbali na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid na NaibuWaziri wa Sheria na katiba, Angela Kairuki (kulia) wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi watu waliozaliwa kwenye hospitali hiyo miaka 25
iliyopita hospitali ilipoanzishwa.
|
|
RAIS HAPO AKIWA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI HIYO |
|
AKIWA NA WANAFAMILIA WA HAYATI PROF. HUBERT KAIRUKI |
|
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya
Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dk Asser Mchomvu akimwelezea Rais jengo la mfano
la Wodi ya wazazi inayotarajiwa kujengwa Hospitalini hapo.
|
|
Mama mzazi wa Hayati Profesa Hubert
Kairuki, Angela Kairuki (kulia), Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela
Kairuki (kushoto) na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda wakipunga mkono
wakati wa sherehe hiyo.
|
|
Rais
Jakaya Kikwete akimkabidhi tuzo mmoja wa wafanyakazi walitimiza miaka 25 kwenye
Hospitali hiyo, Mchungaji Henry Mfuko wakati wa sherehe hiyo. Anayeshuhudia ni Meneja wa
Hospitali hiyo, Gerald Manongi na mwanasiasa mkongwe nchini, Sir George Kahama (kulia). |
|
Rais
Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Muasisi wa Hospitali ya
Kairuki Prof. Hurbert Kairuki wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 25 ya
hospitali hiyo Dar es Salaam. |
|
Rais Jakaya
Kikwete akimkabidhi tuzo Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati wa sherehe za
kuadhimisha miaka 25 ya hospitali hiyo Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti
wa Hospitali hiyo, Kokushubira Kairuki na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk Seif Rashid (mwenye miwani). (Picha na Mpiga Picha Wetu)
|
COMMENTS