Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) Brigedi...
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA
JKT) Brigedia Jenerali Charo Yateri amesema kuwa jitihada na juhudi
zinazofanywa na vijana wake ndicho kitu kikubwa kilichopelekea kupata
tuzo ya masuala ya Kilimo na ufugaji.
Tuzo
hiyo walikabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba
yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Brigedia
Jenerali Yateri alisema kuwa, mbali na kujihusisha na masuala ya
ufugaji na kilimo amvapo wana dhana mbalimbali wanazozitumia ikiwemo
Kilimo cha umwagiliaji pia wanajihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia
ya kisasa ya kuwaweka.
Pmaoja
na hilo, SUMA JKT wamejikita zaidi katika utengenezaji wa samani za
ndani kama makabati, vitanda, samani za maofisini na vitu mbalimbali pia
wanatengeneza nguo mbalimbali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA
JKT) Brigedia Jenerali Charo Yateri akizungumza na Globu ya Jamii mara
baada ya kupata tuzo katika masuala ya Kilimo na ufugaji waliyokabidhiwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika
ufunguzin wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana
kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Dhana
mbalimbali za Kilimo zinazotumika kwa Kilimo cha Umwagiliaji
vinavyotumika na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), dhana hizo ziliweza
kuwekwa wakati wa ufunguzi maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba
yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Baadhi
ya wananchi wakiangalia Mabwawa ya Samaki yanayotumiwa na Jeshi la
Kujenga Taifa (SUMA JKT) kwa ajili ya ufugaji ambapo kila tenki moja
linachukua samaki 100 wakati wa ufunguzi maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Wananchi
wakiangalia mabanda ya kuku wanaofugwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA
JKT) wakati wa ufunguzi maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba
yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Samani
zinazotengenezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) zikiwa katika
banda lao wakati wa ufunguzi maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba
yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
COMMENTS