F TIB CORPORATE BANK KATIKK JUKWAA LA BIASHARA TANGA | Okandablogs

Friday, August 18, 2017

TIB CORPORATE BANK KATIKK JUKWAA LA BIASHARA TANGA Mkurugenzi wa Mkuu wa TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege akizungumza wakati wa Jukwaa la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka akizungumza wakati wa Jukwaa hilo.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiwa na wajumbe wa Jukwaa hilo Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya TSN Limited Dkt. Jimmy Yonazi (wa pili kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege, Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka .

TIB Corporate Bank (TIB CBL) wameshiriki katika Jukwaa la Biashara, Jukwaa hili linakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili na kuona namna gani Kila mmoja anawezesha mkoa wa Tanga Katika kuleta maendeleo.
 
TIB Corporate Bank ni benki ya Biashara na inatoa Huduma zote za kibenki. Kwa kutambua fursa mbalimbali katika Mkoa wa Tanga, benki inajiweka sawa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wanaTanga. Tunambua Kuwa maendeleo yoyote Yale ya kibiashara na viwanda yanahitaji uwezeshwaji wa kifedha (Bank facilities).
 
TIB Corporate Bank  inatoa
Huduma mbalimbali kutokana na mahitaji ya Mteja. Baadhi ya Huduma hizo ni pamoja na akaunti mbalimbali za kwa makampuni na Watu binafsi,mikopo ya aina mbalimbali ya muda mfupi na muda wa kati, dhamana za kibenki (bank guarantee), ununuaji na uuzaji wafedha za kigeni, uwekezaji katika hati fungani (treasury bills & Bonds), ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni
(Cash management) pamoja na ulipaji wa mishahara kwa Njia rahisi na haraka
  
Huduma zetu hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha Mteja anafurahia mahusiano yake na benki.


Pia Huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha zaidi.


(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

0 comments:

Post a Comment