RAIS KIKWETE AUFAGILIA MFUKO WA PENSHENI WA PPF KWA UWEKEZAJI BORA

Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Subira Athumani, mfano wa kadi ya uanachama kupitia mpango wa “Wote Scheme” ambao unahus...




Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Subira Athumani, mfano wa kadi ya uanachama kupitia mpango wa “Wote Scheme” ambao unahusu kujiunga na uanachama kwa uchangiaji wa hiari. (kushoto), ni Naibu waziri wa fedha, Adam Malima, na wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, Dkt. Aggrey Mlimuka
 Rais Jakaya Kikwete, (wa pili kushoto), akiangalia ushuhuda uliokuwa ukitolewa na Mwanachama wa PPF kupitia mpango wa Wote Scheme, baada ya kuweka jiwe la msingi la kitegauchumi la Mfuko huo mjini Mtwara Oktoba 10, 2015. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, Dkt. Aggrey Mlimuka (kushoto), Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngoi (kulia), na Meneja Uhusiano Lulu Mengele.



RAIS Jakaya Kikwete, akitoa hotuba kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la kitegauchumi PPF Plaza eneo la Vigaeni, mjini Mtwara, Oktoba 10, 2015. Jengo hilo la ghorofa  mali ya PPF litagharimu shilingi Bilioni 9.5 ujenzi wake utakapokamilika mwishoni mwa mwaka huu.
 *************
NA K-VIS MEDIA, MTWARA
RAIS Jakaya Kikwete ameumwagia sifa kemkem Mfuko wa Pensehni wa PPF, kwa uwekezaji bora, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jingo la ghrorofatano  la kitegauchumi la PPF Plaza mjini Mtwara Oktoba 10, 2015.

“Nimefurahishwa sana na uwekezaji wenu kwani ninaenda kustaafu na kupumzika kwa raha kutokana na mambo makubwa mliyotafanya, nah ii ni fursa nzuri kwa uwekezaji kwenye mkoa huu ambao utakuwa kitovu cha uchumi.” Alifafanua Rais.

Rais Kikwete, ambaye alitua mkoani humo akitokea nchi I Msumbiji alikokwenda kuaga, alisema, Mtwara yuko muwekezaji ambaye ni tajiri mkubwa barani Afrika akishikilia namba moja, nay eye angependa walau kulala mkoani Mtwara wakati wa ziara zake za kukagua miradi yake, na lakini atalala wapi, wakati hakuna hoteli yenye hadhi yake.? Aliuliza na kuwataka wawekezaji zaidi katika eneo la mahoteli ili kuweza kuwapokea wafanyabiashara wakubwa wanaotembelea Mtwara ivi sasa.

Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Aggrey Mlimuka, alisema, jingo hilo litakapokamilika ujenzi wake litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 9.5 na tayari baadhi ya ghorofa zimeshachukuliwa.

 Rais Jakaya Kikwete, (katikati), akipunga mkono kuwaaga wafanyakazi wa PPF na wajenzi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko huo “PPF PLAZA” baada ya kuweka jiwe la msingi

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akitoa hotuba kumkaribisha Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi la jingo la kitegauchumi la PPF mjini Mtwara Oktoba 10, 2015
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dkt. Aggrey Mlimuka, akitoa hotuba wakati wa uwekaji jiwe la msingi la jingo la kitegauchumi la Mfuko huo mjini Mtwara Oktoba 10, 2015.

 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Dkt. Aggrey Mlimuka, wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanachama mpya wa mpango wa uchagiaji wa hiari (Wote Scheme), wa Mfuko huo, Subira Athumani Makumbiri, baada ya kukabidhiwa mfano wa kadi ya uanachama. (PICHA ZAIDI BOFYA HAPA)
Ngoma za utamaduni nazo zilikuwepo kunogesha shughuli
 Baadhi ya wafanyakazi wa PPF, na wajenzi, waimpungia mkono Rais na ujumbe wake wakati waiondoka eneo la tukio.
 Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. Aggrey Mlimuka, (wane kulia), na wafanyakazi wa PPF, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa uwekezaji, Steven Alfred (wa kwanza kushoto mstari wa mbele)

 Rais Kikwete, na Mama Salma Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa fedha, Adam Malima, Waziri wa Nishati, George Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF, Wafanyakazi wa PPF, na wajenzi wa jingo la kitegauchumi la PPF Plaza mjini Mtwara leo Oktoba 10, 2015. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Sad)
 Rais Jakaya Kikwete, (katikati), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Pensheni wa PPF, Aggrey Mlimuka, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye jingo la kitegauchumi la Mfuko huo, PPF Plaza mjini Mtwara
 Rais akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF, Bi. Amelye
 Rais akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa uwekezaji, Steven Alfred
 Kaimu Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Steven Alfred, akitoa hotuba wakati wa uwekaji jiwe la msingi la jengo la kitegauchumi la Mfuko huo mjini Mtwara Oktoba 10, 2015
Jengo la kitegauchumi la ghorofa 5 linalomilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF, eneo la Vigaeni mkoani Mtwara, ambalo Rais Jakaya Kikwete, ameliwekea jiwe la msingi leo Oktoba 10, 2015

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS KIKWETE AUFAGILIA MFUKO WA PENSHENI WA PPF KWA UWEKEZAJI BORA
RAIS KIKWETE AUFAGILIA MFUKO WA PENSHENI WA PPF KWA UWEKEZAJI BORA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKgYLNN263lAMlk0eFVoFuZZKBrbuf_sFDuOnd1rsS0NVHOt0xwHlQN1yGf7vItBdqV8TFq2EcbLNl8jKw7dF7eic-4wCpy7lLRFqEkalhp_f8pQ8vrejyY79G54mIoYpJ923yJU_sxxoO/s640/JK_New+mwmbwe.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKgYLNN263lAMlk0eFVoFuZZKBrbuf_sFDuOnd1rsS0NVHOt0xwHlQN1yGf7vItBdqV8TFq2EcbLNl8jKw7dF7eic-4wCpy7lLRFqEkalhp_f8pQ8vrejyY79G54mIoYpJ923yJU_sxxoO/s72-c/JK_New+mwmbwe.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/10/rais-kikwete-aufagilia-mfuko-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/10/rais-kikwete-aufagilia-mfuko-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy