WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIAGIZA TAMISEMI KUTENGA MAENEO MAALUMU YA WAMACHINGA
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Bw. Peter Kundy, akielezea kuhusu zoezi la utoaji wa vitambulisho vya uraia katika mkoa wa Dodoma wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), uliofanyika Jijini Dodoma.

HomeJamii

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIAGIZA TAMISEMI KUTENGA MAENEO MAALUMU YA WAMACHINGA

Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameziagiza Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutenga maeneo maalumu kwa aji...

SERIKALI KUWAUNGANISHA WAZALISHAJI WAKUBWA WA CHAKULA KATIKA KATA TANO WILAYANI IRAMBA.
MEYA WA JIJI LA DAR MWITA AWATAKA WANANCHI KUWA WAMOJA BILA KUJALI TOFAUTI ZA ITIKADI ZA VYAMA VYAO
WANADAYASFORA WA MAREKANI WATOA HUDUMA ZA MATIBABU ZANZIBAR


Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameziagiza Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo (Wamachinga) ili waweze kufanya biashara zao bia bughdha yoyote.
Maagizo hayo yametolewa Jijini Dodoma kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Machinga (SHIUMA) na kuongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hao wanashiriki kukuza biashara zao na pato la Taifa.
Dkt. Kijaji alisema kuwa wamachinga na wajasiriamali wengine wanapokosa maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao inakuwa vigumukupata mikopo kutokana na kutotambuliwa, hivyo Sekta za Fedha zikiwemo Benki kuwa na wasiwasi na urejeshwaji wa Fedha hizo hivyo hatua ya kuwatambua itasaidia kutatua changamoto hiyo.
 “Tanzania inatarajia kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025 na wafanyabiashara wakiwemo wamachinga ndio watakaowezesha kufikia lengo hilo kwa kulipa kodi, hivyo Serikali inachokifanya inaweka mazingira mazuri ya kazi kwa wafanya biashara”, alisema Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa baada ya maombi ya muda mrefu ya Wamachinga kutaka kutambuliwa, Serikali katika Sheria ya fedha ya mwaka 2017/18 imeanza kutekeleza maombi hayo kwa kuhakikisha wanatambuliwa na kupewa vitambulisho vya Taifa kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kurahisha utendaji kazi wao hasa na Sekta ya Fedha kwa kupata mikopo.
Dkt. Kijaji ameipongeza Benki ya NMB ambayo imeendelea kukutana na kuwafadhili wafanyabiashara wadogo ukiwemo Mkutano huo wa SHIUMA kwa kuwa wanatekeleza kwa vitendo azma ya Sekta ya Fedha kuwafikia wananchi wa hali ya chini
Aidha, alirejea pongezi zake kwa baadhi ya benki hapa nchini ikiwemo NMB, CRDB na ABC kwa uamuzi wao wa kushusha riba za mikopo yao na kueleza matumaini yake kwamba wamachinga na wajasiriamali wengine watachangamkia fursa za mikopo hiyo.
Alisema Desemba, 2017 Serikali ilizindua Sera ya huduma ndogo za Fedha itakayowezesha kutambua Taasisi zote ndogo za Fedha zinazokopesha wananchi ili ziweze kuzingatia kanuni za utawala bora zitakazosaidia wafanyabiashara wadogo kukopa kwa kufuata sheria ili kuondoa kudhurumiwa.
Aidha amewapongeza wanachama wa SHIUMA kwa kuanzisha umoja wao utakaosaidia Serikali kupeleka huduma kwa urahisi na kwa usahihi kwa manufaa ya wafanyabiashara na Taifa kwa ujumla na akaahidi kuwa Serikali ipo pamoja nao kwa kuwa ni Serikali inayojali wanyonge.
Akizungumza kwaniaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Nchini-IGP Simon Sirro, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi-Lazaro Mambosasa, amewapiga marufuku watu wote wanaopora mali za wamachinga nchi nzima.
Alisema kuwa Jeshi lake litawachukulia hatua kali wale wote watakaojihusisha kwa namna moja au nyingine kunyang'anya ama kutaifisha bidhaa za wafanyabiashara wadogowadogo popote pale kwa kuwa vitendo hivyo havikubaliki.
 “Watu wote waliokuwa wanajipatia mali za wamachinga kwa kuwanyanganya bila kupeleka kwenye Mamlaka husika na badala yake wanauza na kutumia huoni unyang’anyi na atakayefanya hivyo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Alisema Umoja huo wa wamachinga usikubali kushawishiwa kwa nia ovu na watu na baaada ya kujinufaisha binafsi wanawaacha wafanyabiashara hao bila chochote.
Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga Bw. Ernest Masanja alisema kuwa Wanaunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa imeonesha nia ya kuwajali wanyonge hasa wamachinga.
Bw. Masanja alisema katika Mkutano huo wameazimia kushirikiana na TRA wakati wa kutoa semina kuhusu namana ya kulipa kodi na pia wanachama wa vikundi vyote vya wamachinga vilivyo sajiliwa wapewe vitambulisho vya Taifa ili wasajiliwe na Mamlaka hiyo.
Naye Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Bw. Peter Kundy alieleza kuwa mpaka sasa kwa Wilaya ya Dodoma Mjini, zoezi la Uhakiki na uandikishaji kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa imefanyika kwa kata 41 na zimesalia 6 pekee na zoezi lililobaki ni kutoa pingamizi kwa wasio stahili ili ifikapo Desemba zoezi hilo la utoaji vitambulisho litakuwa limekamilika.
Alisema  zaidi ya watumishi mia tano kutoka Idara ya Uhamiaji wamepelekwa nchi nzima ili kuharakisha zoezi la upatikanaji wa vitambulisho hivyo ili kusaidia katika upatikanaji wa mikopo katika sekta za fedha, elimu, afya na hata hati za kusafiria nje ya nchi kwa ajili ya shughuli za uchumi.
Shirika la Umoja wa Wamachinga (SHIUMA), limeanzishwa hivi karibuni likiwa na lengo la kuwaunganisha wafanyabishara wadogo wadogo nchini kote.



Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Kipolisi Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi-Lazaro Mambosasa, akizungumza kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa  Polisi, IGP Simon Sirro, ambaye amepiga marufuku watu wote wanaopora mali za wamachinga nchi nzima, wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Wamachinga nchini (SHIUMA), uliofanyika Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga, Bw. Ernest Masanja akiipongeza Serikali kwa kuwajali wamachinga na kuiomba iwapatie vitambulisho vya Taifa ili wasajiliwe na Mamlaka ya Mapato Tanzania na kuvitumia vitambulisho hivyo kuombea mikopo kwenye taasisi za fedha, wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Wamachinga nchini (SHIUMA), uliofanyika Jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akifunga Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), kwa niaba ya Waziri Mkuu  Mhe. Kassim Majaliwa, Jijini Dodoma, ambapo ameiagiza TAMISEMI, kutenga maeneo maalumu ya Wamachinga.



Baadhi ya wamachinga-Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA) wakisikiliza kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifunga Mkutano Mkuu huo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jijini Dodoma.



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akipeana mkono na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Kipolisi Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi-Lazaro Mambosasa, wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), uliofanyika Jijini Dodoma.


Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (walioketi-katikati), baada ya kufunga rasmi Mkutano Mkuu huo, Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIAGIZA TAMISEMI KUTENGA MAENEO MAALUMU YA WAMACHINGA
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIAGIZA TAMISEMI KUTENGA MAENEO MAALUMU YA WAMACHINGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihH8C51-4tvX0OuzepUmnWg7bLBHJzO-Jt1h9p_J_Fm5zjcm9FQxmQx9zh2PGsP2yAZ8s2kLCNyvQOYFpzwASeoDo4c0GLa-u7Mum0HDaT3Tfnx-wdg4o4T03Iy0BWWzyc7b71Q_hpBYw/s640/AC3A0632.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihH8C51-4tvX0OuzepUmnWg7bLBHJzO-Jt1h9p_J_Fm5zjcm9FQxmQx9zh2PGsP2yAZ8s2kLCNyvQOYFpzwASeoDo4c0GLa-u7Mum0HDaT3Tfnx-wdg4o4T03Iy0BWWzyc7b71Q_hpBYw/s72-c/AC3A0632.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-aiagiza.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-aiagiza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy