WAZIRI MKUU AIPONGEZA BENKI YA NMB KUCHANGIA HUDUMA ZA KIJAMII
HomeJamii

WAZIRI MKUU AIPONGEZA BENKI YA NMB KUCHANGIA HUDUMA ZA KIJAMII

 W aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 10, 000,000/=  kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mku...

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AENDELEA KUWABANA WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA NCHI
WANAWAKE TAA WAUNGANA NA WENZAO MLIMANI CITY DAR ES SALAAM KUADHIMISHA SIKUKU YA WANAWAKE DUNIANI
MDAHALO WAKUWANIA UONGOZI WA URAIS JUMUIYA YA WATANZANIA DMV (PART ONE)



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 10, 000,000/=  kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) ukiwa ni mchango wa Benki hiyo kwa timu ya mpira wa miguu ya Namungo ya wilayani Rungwa. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam Mei 30, 2018. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa NMB,  Vicky Bishubo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bibi Ineke Bussemaker (katikati) na  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa NMB (Head of Government Business), Vicky Bishubo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni  jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) na  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa NMB (Head of Government Business), Bibi Vicky Bishubo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2018.

NA OWM, DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameipongeza Benki ya NMB kwa kuchangia huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo elimu, afya na michezo.

Ametoa pongezi hizo leo (Jumatano, Mei 30, 2018) wakati akizungumza Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker ofisini kwake Magogoni jijini Dra es Salaam. 
Amesema katika jitihada za Serikali za kufufua ushirika na hasa kwenye mazao makuu matano, wakulima wamehamasishwa wafungue akaunti ili malipo ya fedha zao yafanywe moja kwa moja kweye akaunti zao. 
“Tumehamasisha wakulima wote wafungue akaunti ili malipo ya mazao yao yafanywe mojamoja katika akaunti zao jambo ambalo litaepusha wizi au kunyang’anywa fedha wawapo mitaani, na kupitia mawakala walioko vijijini, wataweza kupokea fedha hizo,” amesema.
Amesema uwepo wa mawakala wa benki hadi vijijini, umesaidia kuwafanya Watanzania wasiweke fedha ndani ya nyumba zao.
Akizungumzia mchango wa Benki hiyo kwenye huduma za jamii, Waziri Mkuu amesema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuchangia vitabu, madawati na michezo ambapo imetoa mchango wa sh.milioni kwa timu ya soka ya Namungo iliyoko wilayani Ruangwa.
“Tumeona Benki ya NMB ikifadhili timu mbalimbali za ligi kuu kama vile AZAM, na sasa wameanza kuchangia timu za daraja la kwanza kwa kuichangia timu ya Namungo shilingi milioni 10. Pia walichangia sh.milioni kwenye ujenzi wa uwanja wa kisasa kule Ruangwa, tunawashukuru sana,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Bussemaker alisema wamefurahi kupata fursa ya kuichangia timu ya Namungo na kwamba wataifuatilia kwa karibu kuona ushiriki wake ukoje kwenye ligi hiyo. “Pia tunaitakia kila la kheri kwenye ushiriki wao wa ligi daraja la kwanza,” alisema.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AIPONGEZA BENKI YA NMB KUCHANGIA HUDUMA ZA KIJAMII
WAZIRI MKUU AIPONGEZA BENKI YA NMB KUCHANGIA HUDUMA ZA KIJAMII
https://i.ytimg.com/vi/RZLpR3LBbCU/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/RZLpR3LBbCU/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-mkuu-aipongeza-benki-ya-nmb.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-mkuu-aipongeza-benki-ya-nmb.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy