KATIBU MKUU TARISHI ATETA NA KIKOSI KAZI CHA TUME YA TAIFA YA  UCHAGUZI CHA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akifuatilia  kikao na Kikosi kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi,   leo mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.
HomeJamii

KATIBU MKUU TARISHI ATETA NA KIKOSI KAZI CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI CHA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Na Mwandishi Maalum Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni Taasisi mojawapo iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Ofisi ya Wa...

KANUNI UENDESHAJI MITANDAO YA KIJAMII KUKAMILIKA MAPEMA- DK MWAKYEMBE
TEMESA YAUNDA KIKOSI KAZI KUFUATILIA DENI LA TSH BILIONI 10 KUTOKA TAASISI ZA UMMA
MEM NEWS BULLETIN ISSUE NO: 170


Na Mwandishi Maalum
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni Taasisi mojawapo iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi amekutana na Kikosi Kazi cha Tume hiyo kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma,  lengo ni kuangalia namna serikali inavyoweza kusaidia kwa maeneo inayoruhusiwa  kikatiba katika  kuwasaidia kutekeleza majukumu yake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 5 kifungu kidogo cha 3 (a) ambacho kimeweka uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini na Ibara ya 74 kifungu kidogo cha 6 (a) na (e), kinaipa Tume madaraka ya kuchukua jukumu la kuandikisha wapiga Kura nchini Tanzania.
Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 15 (3) kinaipa madaraka Tume ya Uchaguzi  kutengeneza mfumo na utaratibu wa  uandikishaji wa wapiga Kura nchini na uboreshaji wa daftari hilo mara mbili kati ya Uchaguzi mkuu mmoja na unaofuata.     
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni miongoni mwa Taasisi ambazo zipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi hiyo ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiongoza kikao na Kikosi kazi  cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura walipokutana  leo mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.

Mkurugenzi Idara ya Sera na Bunge Ofisi ya Waziri Mkuu,Yona Mwakilembe akitoa ufafanuzi katika  kikao hicho wakati Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi  kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kilipokutana na Katibu Mkuu (hayupo pichani)   leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.


Baadhi ya wajumbe wa  Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi  kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura wakifuatilia kikao na  Katibu Mkuu (hayupo pichani)  leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KATIBU MKUU TARISHI ATETA NA KIKOSI KAZI CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI CHA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
KATIBU MKUU TARISHI ATETA NA KIKOSI KAZI CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI CHA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgasb_9W8vvm9NIbVIu93LhzGr_anuZATPL01oYbKjxf3_7ln_UOoBAxYtpftBRozB2J3uwhxMZK0aOoaJjg-aAl80jNJKx62tm0C_3Q_8Tx6z7nUMc39c_7MztjIVJqoLbdZaUgaNt_gY/s640/PICHA+NA.+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgasb_9W8vvm9NIbVIu93LhzGr_anuZATPL01oYbKjxf3_7ln_UOoBAxYtpftBRozB2J3uwhxMZK0aOoaJjg-aAl80jNJKx62tm0C_3Q_8Tx6z7nUMc39c_7MztjIVJqoLbdZaUgaNt_gY/s72-c/PICHA+NA.+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/katibu-mkuu-tarishi-ateta-na-kikosi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/katibu-mkuu-tarishi-ateta-na-kikosi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy