WAZIRI KIGWANGALLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KANDA - PORI LA AKIBA RUKWA KUPISHA UCHUNGUZI KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UJANGILI
HomeJamii

WAZIRI KIGWANGALLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KANDA - PORI LA AKIBA RUKWA KUPISHA UCHUNGUZI KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UJANGILI

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA MALIASILI NA UTALII Simu Na: +255 026 2321566 Nukushi: +255 026 2321514 Barua pepe: p...


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Simu Na: +255 026 2321566
Nukushi: +255 026 2321514
Barua pepe: ps@mnrt.go.tz
      
Mtaa wa Kilimani,
Barabara ya Askari,
S.L. P 1351,
40472-DODOMA

MKUU WA KANDA - PORI LA AKIBA RUKWA ASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (Mb) amemsimamisha kazi Bwana Emmanuel Barabara, Mhifadhi Wanyamapori Mkuu ambaye pia ni Mkuu wa Kanda – Pori la Akiba Rukwa, lililopo wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi, kuanzia jana tarehe 10 Machi, 2018 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Dk. Kigwangalla amechukua uamuzi huo kufuatia taarifa za raia wema kuwa Bwana Barabara amekuwa akishirikiana na majangili katika kuhujumu rasilimali za misitu nchini.

Aidha, Waziri Kigwangalla ameagiza iundwe Kamati ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo, na endapo mtuhumiwa huyo atakutwa na hatia, hatua kali za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma ili iwe fundisho kwa wengine.

Tunatoa onyo kali kwa watumishi wa Wizara wanaojihusisha na vitendo vya uhujumu wa rasilimali za Misitu, Wanyamapori na Malikale kuacha mara moja kwani hatutosita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo ikiwemo kufukuzwa kazi.

Watumishi wote wa Wizara wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyowekwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya uhifadhi wa rasilimali za nchi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. 



Dk. Aloyce K. Nzuki
KAIMU KATIBU MKUU

11 Machi, 2018

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI KIGWANGALLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KANDA - PORI LA AKIBA RUKWA KUPISHA UCHUNGUZI KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UJANGILI
WAZIRI KIGWANGALLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KANDA - PORI LA AKIBA RUKWA KUPISHA UCHUNGUZI KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UJANGILI
https://lh3.googleusercontent.com/U695KwPU_9_cxd8Q-zcUnbbPn-g-YGVqOvpV_mA5QjM97B0wqChFpKBwiQghTvt8UIn58cwx0LPQpMI307hxocuiIPzKOHt0jaykQ52uwVTElVvhJbx5rnuFMsGTtasFKpOoE2_ALOfquQ7AAg
https://lh3.googleusercontent.com/U695KwPU_9_cxd8Q-zcUnbbPn-g-YGVqOvpV_mA5QjM97B0wqChFpKBwiQghTvt8UIn58cwx0LPQpMI307hxocuiIPzKOHt0jaykQ52uwVTElVvhJbx5rnuFMsGTtasFKpOoE2_ALOfquQ7AAg=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-kigwangalla-amsimamisha-kazi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-kigwangalla-amsimamisha-kazi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy