WAZIRI JAFO AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA UJIJI NA PANGANI
HomeJamii

WAZIRI JAFO AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA UJIJI NA PANGANI

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO DAR ES SALAAM 27.3.2018 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),...

ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JKT 2017
TAARIFA YA UMMA. NGO'S ZINAZOTARAJIWA KUFUTIWA USAJILI HIZI HAPA
MAKINDA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA KUJADILI MAENDELEO YA TANZANIA NA KOREA


Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
27.3.2018

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amewasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Kigoma Ujiji na Pangani Tanga kutokana na Ofisi zao kupata hati chafu katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne (Machi 27, 2018), Waziri Jafo alisema Ofisi yake imetekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe kuhusiana na ripoti ya CAG kuwataja Watendaji hao kuzembea na kusababisha taasisi zao kupata hati chafu.
Aliwataja Wakurugenzi waliosimamishwa kazi na kupisha uchunguzi kuwa ni Bi. Hanji Godigodi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Bw. Sabas Damian Chambasi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
“Namwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI aunde timu ya Wataalamu kuchunguza utendaji kazi wa Wakurugenzi hao na kunipatia taarifa ndani ya wiki tatu kuanzia leo” alisema Waziri Jafo.
Kuhusu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, Bw. Judethadeus Mboya ambaye kustaafu utumishi, Waziri Jafo alisema uchunguzi dhidi yake utaendelea kufanyika ili kubainisha kuhusika kwake katika kuisababishia halmashauri hiyo kupata hati chafu.
Akifafanua zaidi Waziri Jafo alisema katika taarifa hiyo ya CAG ya mwaka 2016/17, ripoti hiyo ilibainisha kuwa katika ngazi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuliwepo na jumla ya vitabu 379 vya makusanyo ya mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa CAG kwa ajili ya kufanyika ukaguzi wa mahesabu yake.
Aliongeza kuwa kutokana na taarifa hiyo, Ofisi yake itawasiliana na Wakurugenzi wote kuhakikisha kuwa inawasilisha vitabu hivyo vyenye taarifa na nyaraka za ukaguzi katika ofisi ya CAG haraka iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa Jafo alisema kwa sasa Serikali imepata mafanikio makubwa sana katika suala zima la udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali katika mamlaka za Serikali za Mitaa ikilinganisha na miaka ya nyuma ambao hali ya matumizi haikuwa nzuri.
Waziri Jafo alizipongeza Halmashauri 166 zilizopata hati safi na kuendelea kufanya vizuri katika kusimamia taratibu za matumizi ya fedha za umma pamoja na kuzitaka halmashauri 16 zilizopata hati isiyoridhisha kufanya maboresho katika utendaji kazi ili kupata hati safi.
“Kwa upande wa Halmashauri zilizopata hati chafu naziagiza zibadilishe mienendo ya utendaji kazi katika halmashauri zao sambamba na kuyaagiza Mabaraza ya Madiwani kusimamia vyema Halmashauri hizi katika mipango ya matumizi ya fedha za Serikali” alisema Jafo.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI JAFO AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA UJIJI NA PANGANI
WAZIRI JAFO AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA UJIJI NA PANGANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8yEA7chNOdHSMIVF-FxVdJno9p6rUNUeq4dorNNmXu3e7nK0TlSVxhNJxfPKS1tDj2VvU0d1BsuUvMA1NfwdyaSszlp21K3j7w7crXjnc-nyNVs6kik8KW7AQuCRNWsqgLjgnd3Szlis/s400/1+%252811%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8yEA7chNOdHSMIVF-FxVdJno9p6rUNUeq4dorNNmXu3e7nK0TlSVxhNJxfPKS1tDj2VvU0d1BsuUvMA1NfwdyaSszlp21K3j7w7crXjnc-nyNVs6kik8KW7AQuCRNWsqgLjgnd3Szlis/s72-c/1+%252811%2529.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-jafo-awasimamisha-kazi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-jafo-awasimamisha-kazi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy