NAIBU WAZIRI MAVUNDE AHAMISHIA OPERESHENI YA KUWABAINI WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA KAZI MKOANI MOROGORO
HomeJamii

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AHAMISHIA OPERESHENI YA KUWABAINI WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA KAZI MKOANI MOROGORO

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwand...

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA MELI YA HOSPITALI YA CHINA, AAGANA NA KUSHUKURU WANAMAJI NA MADATARI WALIOKUJA NAYO
TBL YAJITOSA KATIKA KAMPENI ZA KUPINGA UKATILI WA JINSIA
VIJANA WASOMI WATAKIWA KUMSAIDIA RAIS MAGUFULI KULILETEA TAIFA MAENDELEO

 Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony
Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Tumbaku Alliance One Mkoani
Morogopro leo Machi 9, 2018. Mhe. Mavunde ameagiza waajiri 242 Mkoani Morogoro ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) kufikishwa mahakamani mara moja.




NA
K-VIS BLOG, Morogoro
OPERESHENI
ya nchi nzima kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi
sheria
ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa
Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), inayoongozwa na
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, imeingia
Mkoani Morogoro leo Machi 9, 2018, ambapo waajiri wamechukuliwa hatua
mbalimbali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.
Operesheni
hiyo iliyoanzia jijini Mwanza Februari 26, 2018 inafuatia agizo alilolitoa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, jijini Mbeya mwishoni mwa mwaka jana ambapo
aliagiza waajiri ambao bado hawajatekeleza Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi,
Sura 263 marejeo ya mwaka 2015, ambayo inamtaka kila mwajiri kutoka sekta ya
umma na binafsi Tanzania bara awe amejisajili na kuwasilisha michango kwenye
Mfuko huo, wafikishwe mahakamani.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa
Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, ambaye anafuatana na Mhe.
Mavunde kwenye ziara hiyo ya kushtukiza, kuna jumla ya waajiri 536, na kati ya
hao ni waajiri 294 tu ndio waliojisajili na Mfuko huku wengine 242 bado
hawajatekeleza takwa la kisheria la kujisajili na Mfuko.
“Naagiza
waajiri hawa ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi,
wanaofikia 242 wafikishwe mahakamani mara moja ili wakajibu mashtaka kwanini
hawajatimiza wajibu wao wa kisheria.” Aliagiza Mhe. Mavunde.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza, mjini
Morogoro, Mhe. Mavunde ameiagiza WCF kuwafikisha mahakamani mara moja, waajiri
wa kampuni ya Sengo 2000 Tanzania Limited, na Midland Inn Lodge kutojisajili na
Mfuko.
Huku
kampuni za Hood Transport Company Limited na Alliance One, wao wamekiuka sheria
ya kazi na mahusiano kazini.
“Lakini
pia naagiza waajiri hawa 242 ambao bado hawajajisajili na Mfuko nao wafikishwe
mahakamani mara moja ili wakajibu mashtaka kwanini hawajatimiza wajibu wao wa
kisheria.” Aliagiza Mhe. Mavunde.
Mhe.
Mavunde pia ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko
haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri
anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko.
“Ni
kosa la jinai kwa mwajiri kutotekeleza takwa hilo la kisheria na kifungu cha
71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina
hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo
kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja, kwa hivyo nitoe wito kwa
waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria.­­
Aidha Mhe. Mavunde amerejea kauli yake kuwa nia ya serikali sio
kuwanyanyasa waajiri au kuwapeleka mahakamani.
“Serikali inataka ninyi waajiri mfanye shughhuli zenu za biashara
na uwekezaji na kazi ya kuwahudumia wafanyakazi wenu wanapopatwa na madhara
wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi, jukumu hilo lisimamiwe na Serikali
kupitia Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Naibu Waziri pia amebaini kuwa waajiri katika viwanda hivyo
hawatekelezi sheria ya ajira na mahusiano kazini ambapo ukiukwaji mkubwa wa
sheria hiyo umedhihirika ambapo amewakuta wafanyakazi wakifanya kazi bila ya
vifaa vya kujihami, (protective gears), kufanya kazi kwa masaa mengi kupitia
kiasi, lakini pia wengi wao hawana mikataba ya kazi.
“Tumebaini
kuna mapungufu makubwa sana ya sheria za kazi hasa sheria namba 6 ya mwaka
2004, sheria hii inaelekeza mwajiri azingatie muda wa masaa ya kazi, atoe
mikataba kwa wafanyakazi wote,” alisema Mheshimiwa Mavunde.
Aidha
Kamishna wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa, amesema, Waajiri ni sharti watoe mikataba
kwa wafanyakazi inayoonyesha ni muda gani wa kufanya kazi, likizo kwa
mfanyakazi, na hata kama mfanyakazi analipwa kwea siku ni sharti mambo hayo
yazingatiwe.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi,
(WCF), Bi. Rehema Kabongo, amesema Mfuko umjiandaa kabisa, na maagizo ya
Mheshimiwa Naibu Waziri yatatekelezwa haraka na tayari baadhi ya maeneo hatua
za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi ya waajiri ambao wameshindwa kutekeelza
takwa la kisheria.
“Operesheni
hii ni endelevu tutahakikisha waajiri wote tunawafikia na nitoe rai tu kwa wale
ambao bado hawajajisajili, wasisubiri kupelekewa hati za mashtaka, kwani lengo
la Mfuko ni kuwasidia waajiri kuondokana na jukumu la kuwahudumia wafanyakazi
wao wanapopatwa na madhara mahala pa kazi kwani jukumu hilo kwa sasa kwa mujibu
wa sheria ni la Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi WCF na si mahala pengine
popote.” Alifafanua Bi. Rehema.


Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony
Mavunde, (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi, kiwanda cha
Tumbaku Mkoani Morogoro, Ujaicy Kayera leo Machi 9, 2018 wakati wa ziara yake
ya kushtukiza aliyoifanya Mkoani humo ili kubaini waajiri ambao bado
hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na wale ambao
hawatekelezi Sheria ya Kazi na Mabhusiano Kazini. Mhe. Mavunde ameagiza waajiri
242 ambao hawajajisajili na Mfuko kufikishwa mahakamani mara moja.
  Naibu
Waziri Antoni Mavundeakizungumza na Meneja wa Kampuni ya Hood, Faisal Hood.
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi,
(WCF), Bi.Rehema Kabongo


  Naibu
Waziri akiwasli kwenye Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo
Kingolwira, ambapo alizungumza na wafanyakazi na kubaini makosa ya kiutendaji
kwa muajili.


  Naibu
Waziri akiwasli kwenye Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo
Kingolwira, ambapo alizungumza na wafanyakazi na kubaini makosa ya kiutendaji
kwa muajili.


  Naibu
Waziri akiwasli kwenye Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo
Kingolwira, ambapo alizungumza na wafanyakazi na kubaini makosa ya kiutendaji
kwa muajili.


  Mkurugenzi
wa Rasilimaliwatu, Blasius Lupenza akielezea baadhi ya mikataba ya wafanyakazi
wake kwa Mhe Naibu Waziri katika Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance
kilichopo Kingulwira.




  Naibu Waziri akiangalia Salary slip ya mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Tumbaku.




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NAIBU WAZIRI MAVUNDE AHAMISHIA OPERESHENI YA KUWABAINI WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA KAZI MKOANI MOROGORO
NAIBU WAZIRI MAVUNDE AHAMISHIA OPERESHENI YA KUWABAINI WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA KAZI MKOANI MOROGORO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgI5eKN5vPaGld6mkfmfxCGDNMGdTCnRgmKs0kAqnhPLYePKpfximQPBKPA_xYxHXoKmUZvFT0x-LiJAjHYu0qBNVS53n4ew98V2eSF2P5D0FJ-OAMtCvWr72sXmgDE7Sc6YiNeRatDqNA/s640/5a.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgI5eKN5vPaGld6mkfmfxCGDNMGdTCnRgmKs0kAqnhPLYePKpfximQPBKPA_xYxHXoKmUZvFT0x-LiJAjHYu0qBNVS53n4ew98V2eSF2P5D0FJ-OAMtCvWr72sXmgDE7Sc6YiNeRatDqNA/s72-c/5a.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/naibu-waziri-mavunde-ahamishia.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/naibu-waziri-mavunde-ahamishia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy